Magufuli atengua madai ya kufuta mafunzo ya cheti,

October 6, 2020

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Magufuli, amewataka walimu kupuuzia taarifa ambazo zimetolewa hii leo Oktoba 5, 2020, zikidai kuwa serikali imefuta mafunzo ya ualimu wa shule ya msingi na awali kwa ngazi ya cheti.

Rais Magufuli ametoa kauli hiyo hii leo Oktoba 5, 2020,wakati akizungumza kwa njia ya simu baada ya kumpigia Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Jenista Mhagama katika kongamano la kuadhimishwa simu ya Mwalimu Duniani lililoandaliwa na Chama Cha Walimu (CWT), jijini Dodoma.

“Kuna tangazo moja linazungukazunguka linasema walimu wa cheti zipuuzwe hizo taarifa, tumeanza na ninyi walimu, tutamaliza na ninyi walimu, yaani walimu wote kuanzia ngazi ya cheti mpaka wa juu, hata mke wangu ni mwalimu wa cheti, mke wa Majaliwa naye ni mwalimu wa cheti, kwahiyo walimu wa cheti tunawathamini kama wengine”, amesema Rais Magufuli.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *