Magufuli asema atahakikisha analinda kulinda Muungano,

October 3, 2020

 

MGOMBEA wa Urais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi  ya  chama cha Mapinduzi CCM,Dk. John Pombe Magufuli, amesema kwamba iwapo atachaguliwa kuwa Rais atahakikisha analinda,anadumisha na kuenzi Muungano wa Tanganyika  na Zanzibar pamoja na kulinda mapinduzi matukufu ya Zanzibar   ya mwaka 1964.

Magufuli amesema Muungano wa Tanganyika na Zanzibar unafaida kubwa katika kuleta ustawi wa maendeleo wa Tanzania kwa ujumla  hivyo iwapo atateuliwa na wananchi kuendelea kuongoza miaka 5 mingine atahakikisha analinda,anadumisha na kuenzi Muungano huo sambamba na maoinfuzi matukufu ya Zanzibar.

Hayo ameyaeleza leo wakati akiwahutubia maelfu ya wanachama wa chama cha Mapinduzi visiwani Zanzibar  katika mkutano wa Kampeni uliofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja Mjini magharib Unguja.

Magufuli amesema iwapo wananchi wataendelea kumuamini na kumchagua kuendelea na kuongoza Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania  atahakikisha anaenzi na kudumisha muungano wa Tanganyika na Zanzibar  ambao umeasisiwa na Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere pamoja na Hayati Sheikh Abeid Amani Karume.

DK Magufuku amesema Muungano huo unamanufaa makubwa kwa ustawi wa maendeleo ya Zanzibar  na Tanzania  bara hivyo atahakikisha anaulinda na kuuwenzi.

Aidha Dk Magufuli  amewataka wananchi wazanzibar kumchaguwa mgombea uraisi kwa tiketi ya Chama Cha mapinduzi dk hussein ali hassan mwinyi kwani ndie kiongozi ambae atakaeendeleza yale yote ambayo ameacha raisi wa awamu ya saba kwa kuyatekeleza kwa kishindo.

Kwa upande wake mgombea wa zanzibar kwa tiket ya chama cha mapinduzi  dk hussein  ali hassan mwinyi amesema ataendeleza yale yote ambayo raisi wa awamu ya saba ameyaacha ikiwemo,umeme,maji,sekta ya uvuvi,na uchumi wa bluu

katika mkutano huo raisi wa zanzibar na mwenyekiti wa baraza la mapinduzi dk ali mohammed  shein amewataka wananchi kuwachaguwa viongozi wote wa wilii wazanzibar na wa jamuhuri ya muungano wa tanzani kwa lengo la kuyaendeleza yale yote mazuri ili wananchi waweze kufaidika na mazuri hayo.

Sambamba na hayo raisi magufuli amewataka wananchi kuendeleza kudumisha amani na itulivu wa  nchi yao haswa kufikia uchaguzi mkuu 2020.

Mkutano huo umehudhuriwa na maelfu ya Wapenzib na Wanamchama wa Chama cha Mapinduzi CCM visiwani Zanzibar  huku wasanii mbalimbali wa bongo fleva wakiwabirudisha katika Mkutano huo.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *