Magufuli Ampigia Simu Dkt Mwinyi…

October 14, 2020

Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.John Magufuli, amewaomba wananchi wa Pemba kumchagua yeye na Dkt. Hussein Mwinyi, ili kwa pamoja wazitatue changamoto za maji, ajira na barabara zinazokikabili kisiwa hicho.

Kushoto ni mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Magufuli na kulia ni mgombea urais wa Zanzibar, Dkt Hussein Mwinyi.

Akizungumza kwa njia ya simu na wananchi waliokusanyika katika mkutano wa kampeni katika viwanja vya Mchanga Mdogo wilaya ya Wete, mkoa wa Kaskazini Pemba jana, Dkt. Magufuli, amewahakikishia wananchi wa kisiwa hicho kuwa mambo yote yaliyotajwa kwenye ilani ya uchaguzi ya CCM watayatekeleza kwa ukamilifu.

Katika salamu zake za awali Dkt. Magufuli ameahidi kukitembelea kisiwa hicho cha Pemba mara tu baada ya uchaguzi mkuu kumalizika.

Kwa upande wake mgombea urais wa Zanzibar, Dkt. Hussein Mwinyi, amewaomba wananchi wa kisiwa cha Pemba na Zanzibar kwa ujumla, kuwapuuza wanaodai kuwa Muungano ndiyo chanzo cha kuzorota maendeleo ya visiwa hivyo kwa kusema huo ni upotoshaji.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *