Magufuli ametuinua na kutupa heshima Dodoma, Lazima tumpigie kura za kishindo- Ditopile, on September 17, 2020 at 6:00 am

September 17, 2020

 WANANCHI wa Mkoa wa Dodoma wameaswa kujitokeza kwa wingi Oktoba 28 mwaka huu kumpigia kura nyingi za ndio mgombea Urais kupitia Chama cha Mapinduzi CCM, Dk John Magufuli kutokana na mambo makubwa aliyoyafanya kwenye mkoa huo kwa kipindi cha miaka mitano ya uongozi wake.Hayo yamesemwa na Mgombea Ubunge wa Viti Maalum Wanawake Mkoa wa Dodoma, Mariam Ditopile alipokua kwenye ziara ya vikao vya ndani Wilayani Kongwa alipoenda kumuombea kura Dk John Magufuli na madiwani wa Kata za Jimbo hilo.Kongwa ndio jimbo la Spika wa Bunge na Mjumbe wa Kamati Kuu ambaye tayari ameshapita bila kupingwa hivyo Ditopile amewaomba wananchi wa Kongwa kumpa heshima Magufuli ya kumchagua kwa kishindo.” Dodoma tuna kazi kubwa sana ya kuhakikisha tunaongoza kwa kura za Rais, kwa miaka mitano ya kwanza ya Magufuli ni wazi Sisi ni Mkoa tulionufaika nae kwa kiasi kikubwa, amefanya mambo ambayo hayajawahi kufanyika kwa miaka yote.Kwanza amehamishia Makao Makuu hapa Dodoma pamoja na serikali yote na yeye akiwepo, hapa Kongwa yenyewe mmejengewa vituo vitatu vya afya na sasa kuna Chuo cha Ufundi kikubwa Kabisa cha Veta kinajengwa na kiko tayari kukamilika, mnataka tupewe nini zaidi Ndugu zangu?,” Amesema Ditopile.Amewaomba wanawake wa Umoja wa Wanawake wa CCM Wilaya ya Kongwa kuongoza mapambano ya kutafuta kura za Rais na madiwani na kuhakikisha wagombea wao wote wanaibuka na ushindi mkubwa ili waweze kushirikiana kusongesha maendeleo.Amewataka wana-CCM kuepuka makundi na misuguano katika kipindi hiki cha kampeni badala yake wajikite kuhamasisha wananchi kwenda kupiga kura huku wakieleza mambo yote mazuri ambayo yamefanywa na serikali kwa kipindi cha miaka mitano.Akiwa ziarani Kongwa, Ditopile pia ameshiriki msiba wa mwanachama mkongwe wa CCM katika eneo la Sabasaba, Mzee Yona Lengwale aliyefariki akiwa na miaka 100.” Kwa niaba ya Chama chetu na Mbunge wa Jimbo, Spika Ndugai nimekuja hapa kuungana na nyinyi na kutoa rambirambi zetu, tunauheshimu mchango wa Mzee wetu Yona kwa Nchi yetu na chama pia, niwahakikishie kuwa tutaendelea kuyaenzi mazuri yake lakini pia kuwa na familia yake katika kipindi hiki kigumu.,

 

WANANCHI wa Mkoa wa Dodoma wameaswa kujitokeza kwa wingi Oktoba 28 mwaka huu kumpigia kura nyingi za ndio mgombea Urais kupitia Chama cha Mapinduzi CCM, Dk John Magufuli kutokana na mambo makubwa aliyoyafanya kwenye mkoa huo kwa kipindi cha miaka mitano ya uongozi wake.

Hayo yamesemwa na Mgombea Ubunge wa Viti Maalum Wanawake Mkoa wa Dodoma, Mariam Ditopile alipokua kwenye ziara ya vikao vya ndani Wilayani Kongwa alipoenda kumuombea kura Dk John Magufuli na madiwani wa Kata za Jimbo hilo.

Kongwa ndio jimbo la Spika wa Bunge na Mjumbe wa Kamati Kuu ambaye tayari ameshapita bila kupingwa hivyo Ditopile amewaomba wananchi wa Kongwa kumpa heshima Magufuli ya kumchagua kwa kishindo.

” Dodoma tuna kazi kubwa sana ya kuhakikisha tunaongoza kwa kura za Rais, kwa miaka mitano ya kwanza ya Magufuli ni wazi Sisi ni Mkoa tulionufaika nae kwa kiasi kikubwa, amefanya mambo ambayo hayajawahi kufanyika kwa miaka yote.

Kwanza amehamishia Makao Makuu hapa Dodoma pamoja na serikali yote na yeye akiwepo, hapa Kongwa yenyewe mmejengewa vituo vitatu vya afya na sasa kuna Chuo cha Ufundi kikubwa Kabisa cha Veta kinajengwa na kiko tayari kukamilika, mnataka tupewe nini zaidi Ndugu zangu?,” Amesema Ditopile.

Amewaomba wanawake wa Umoja wa Wanawake wa CCM Wilaya ya Kongwa kuongoza mapambano ya kutafuta kura za Rais na madiwani na kuhakikisha wagombea wao wote wanaibuka na ushindi mkubwa ili waweze kushirikiana kusongesha maendeleo.

Amewataka wana-CCM kuepuka makundi na misuguano katika kipindi hiki cha kampeni badala yake wajikite kuhamasisha wananchi kwenda kupiga kura huku wakieleza mambo yote mazuri ambayo yamefanywa na serikali kwa kipindi cha miaka mitano.

Akiwa ziarani Kongwa, Ditopile pia ameshiriki msiba wa mwanachama mkongwe wa CCM katika eneo la Sabasaba, Mzee Yona Lengwale aliyefariki akiwa na miaka 100.

” Kwa niaba ya Chama chetu na Mbunge wa Jimbo, Spika Ndugai nimekuja hapa kuungana na nyinyi na kutoa rambirambi zetu, tunauheshimu mchango wa Mzee wetu Yona kwa Nchi yetu na chama pia, niwahakikishie kuwa tutaendelea kuyaenzi mazuri yake lakini pia kuwa na familia yake katika kipindi hiki kigumu.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *