Magavana 12 wa Democrat waapa kuwa kila kura itahisabiwa,

October 1, 2020

 

Magavana kumi na mbili wa chama cha Democrat nchini Marekani wametowa tamko la pamoja katika kile wanachosema ni kuilinda demokrasia, wakiapa kwamba kila kura itahisabiwa kwenye uchaguzi mkuu wa Novemba 3, muda mchache baada ya Rais Donald Trump kuonesha kutokuwa na imani na mfumo wa uchaguzi kwenye mdahalo wa kwanza wa ana kwa ana na hasimu wake, Joe Biden. 

Kwenye mdahalo huo wa jana usiku, Trump alidai kwamba upigaji kura kwa njia ya barua, ambao umekuwa maarufu zaidi sasa kwa sababu ya janga la virusi vya corona, una mazingira yote ya wizi, na akakataa kutamka kwamba atayakubali matokeo. 

Pia Trump aliwatolea wito wafuasi wake kuzipima vikali taratibu za upigaji kura kwenye vituo, kauli ambayo wakosoaji wake wanasema inaweza kutumika kuwatisha wapigakura. 

Magavana hao wamesema kwamba kila kura itahisabiwa na endapo Trump atashindwa, watahakikisha anaondoka madarakani.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *