Maelfu waandamana mashariki mwa Urusi kwa Jumamosi ya nane mfululizo, noreply@blogger.com (Muungwana Blog), on August 29, 2020 at 3:00 pm

August 29, 2020

Maelfu ya watu mashariki mwa Urusi wamefanya maandamano leo, ikiwa ni mara ya nane mfululizo mwishoni mwa kila juma- kulalamikia kufungwa jela kwa gavana wa zamani wa jimbo la Khabarovsk.Video na picha zimeonesha umati wa watu wakiwa na mabango na bendera ukipita katika mitaa ya mji huo wa karibu na pwani ya Pasifik nchini Urusi. Baraza la mji wa Khabarovsk lilisema watu 1,200 waliandamana likiongeza kuwa idadi ya waandamanaji inaendelea kupungua katika maandamano hayo ya kila wiki.Wanahabari huru waliokuwa eneo hilo walikadiria kuwa kulikuwa na maelfu ya watu. Gavana wa zamani Sergei Fugal alikamatwa zaidi ya mwezi mmoja uliopita. Yuko rumande mjini Moscow.Wapelelezi wanamtuhumu kwa kuidhinisha mauwaji ya watu wawili wakati akiwa mfanyabiashara miaka 15 iliyopita. Katika kesi nyigine, anatuhmiwa kwa jaribio la kuuwa. Gavana huyo mwenye umri wa miaka 50 anakanusha madai hayo.,

Maelfu ya watu mashariki mwa Urusi wamefanya maandamano leo, ikiwa ni mara ya nane mfululizo mwishoni mwa kila juma- kulalamikia kufungwa jela kwa gavana wa zamani wa jimbo la Khabarovsk.

Video na picha zimeonesha umati wa watu wakiwa na mabango na bendera ukipita katika mitaa ya mji huo wa karibu na pwani ya Pasifik nchini Urusi. Baraza la mji wa Khabarovsk lilisema watu 1,200 waliandamana likiongeza kuwa idadi ya waandamanaji inaendelea kupungua katika maandamano hayo ya kila wiki.

Wanahabari huru waliokuwa eneo hilo walikadiria kuwa kulikuwa na maelfu ya watu. Gavana wa zamani Sergei Fugal alikamatwa zaidi ya mwezi mmoja uliopita. Yuko rumande mjini Moscow.

Wapelelezi wanamtuhumu kwa kuidhinisha mauwaji ya watu wawili wakati akiwa mfanyabiashara miaka 15 iliyopita. Katika kesi nyigine, anatuhmiwa kwa jaribio la kuuwa. Gavana huyo mwenye umri wa miaka 50 anakanusha madai hayo.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *