Madiwani wa CHADEMA walikuwa mabubu: Bi. Afisa Galyatano, on September 11, 2020 at 3:35 pm

September 11, 2020

Na Clavery Christian Biharamulo Kagera.Aliyekuwa Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Biharamulo mkoani Kagera Bi. Afisa Galyatano amewata wanabiharamulo kihakikisha wanawachagua madiwani wa CCM na mbunge wa CCM na Rais wa Chama cha mapinduzi kwakuwa wakifanya hivyo wataweza kujenga umoja utakao wawezesha kupata maendeleo kwa haraka jimboni kwao.Akihutubia katika ufunguzi wa mkutano wa chama ca mapinduzi wilayani Biharamulo ambapo amesema kuwa madiwani wa CHADEMA waliyokuwepo walikuwa mabubu katika vikao vya baraza na walikuwa hawawatetei wananchi wake hali ambayo ilipelekea wilaya hiyo kurudi nyuma kimaendeleo kwasababu ya madiwani ambao hawakuwa na umoja katika kufanya maamuzi kwenye vikao vya baraza.,

Na Clavery Christian Biharamulo Kagera.
Aliyekuwa Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Biharamulo mkoani Kagera Bi. Afisa Galyatano amewata wanabiharamulo kihakikisha wanawachagua madiwani wa CCM na mbunge wa CCM na Rais wa Chama cha mapinduzi kwakuwa wakifanya hivyo wataweza kujenga umoja utakao wawezesha kupata maendeleo kwa haraka jimboni kwao.

Akihutubia katika ufunguzi wa mkutano wa chama ca mapinduzi wilayani Biharamulo ambapo amesema kuwa madiwani wa CHADEMA waliyokuwepo walikuwa mabubu katika vikao vya baraza na walikuwa hawawatetei wananchi wake hali ambayo ilipelekea wilaya hiyo kurudi nyuma kimaendeleo kwasababu ya madiwani ambao hawakuwa na umoja katika kufanya maamuzi kwenye vikao vya baraza.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *