Madagascar yaondoa hatua ya kutotoka nje usiku iliyowekwa kwasababu ya Covid-19,

October 6, 2020

Madagascar iliweka sheria ya kutotoka nje usiku kwasababu ya kuongezeka kwa idadi ya maambukizi ya virusi vya corona.Image caption: Madagascar iliweka sheria ya kutotoka nje usiku kwasababu ya kuongezeka kwa idadi ya maambukizi ya virusi vya corona.

Rais wa Madagascar Andry Rajoelina ameondoa hatua ya kusalia ndani usiku iliyowekwa kukabiliana na usambaaji wa virusi vya corona.

Rais alitangaza kwamba shughuli za michezo zitaruhusiwa lakini kwa idadi ya watu isiozidi 200.

Aidha, watu wanaopanda ndege kwa safari za ndani ya nchi watahitajika kupimwa kuthibitishwa kuwa hawana virusi vya corona saa 48 kabla ya kuondoka na mtu ataruhusiwa tu kupanda ndege ikiwa atathibitishwa kuwa salama dhidi ya virusi hivyo.

Uwanja wa ndege mmoja tu ndio ulioidhinishwa kwa ajili ya safari za ndege za kimataifa mwezi huu kukiwa na miongozi mikali iliyowekwa kuzuia kusambaa kwa virusi vya corona.

Kuvaa barakoa na hatua ya kutokaribiana bado vinaendelezwa kote nchini humo.

Madagascar ilirekodi idadi kubwa ya virusi vya corona mnamo mwezi Julai na kulazimisha serikali kuanzisha tena hatua ya kutotoka nje katika mji mkuu wa Antananarivo.

Rais Rajoelina alikuwa amepigia debe matumizi ya dawa ya miti shamba ambayo alisema kwamba inatibu virusi vya corona vya Covid-19 lakini Shirika la Afya Duniani limedumisha kwamba hakuna tiba ya ugonjwa huo.

Dawa hiyo sasa hivi inatengenezwa kwa muundo wa vidogo na inaendelea kugawanywa kote nchini humo.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *