Macron amtaka Putin kuzungumza na kiongozi wa upinzani Belarus,

October 1, 2020

 

Rais wa Ufaransa Emmanuel Marcon amezungumza kwa njia ya simu na mwenzake wa Urusi Vladimir Putin na kumtaka kufanya mazungumzo na kiongozi wa upinzani wa Belarus Sviatlana Tsikhanouskaya. 

Taarifa iliyotolewa leo na ofisi ya rais wa Ufaransa imesema Macron ambaye hivi karibuni alikutana na Tsikhanouskaya, amemweleza Putin kuwa kiongozi huyo wa upinzani yuko tayari kwa mazungumzo na kumsihisi kutumia nafasi iliyojitokeza. 

Kulingana na taarifa hiyo, Macron na Putin pia wameunga mkono pendekezo la kutafuta usuluhishi wa mzozo wa Belarus kupitia shirika la usalama na ushirikano la Ulaya, OSCE. 

Belarus ni mshirika wa karibu wa Urusi, na Moscow inamuunga mkono rais Alexander Lukashenki aliyetangazwa mshindi wa uchaguzi wa mwezi Agosti ambao mataifa ya magharibi na upinzani wanasema uligubikwa na wizi wa kura.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *