Macron amtaka Putin kuelezea anayoyajua kuhusu tukio la jaribio la mauaji ya mwanasiasa wa upinzani Navalny, on September 14, 2020 at 5:00 pm

September 14, 2020

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amemtolea wito mwenzake wa Urusi Vladimir Putin kutoa ufafanuzi haraka juu ya jaribio la mauaji dhidi ya mwanasiasa wa upinzani Alexei Navalny baada ya uchunguzi uliofanywa na Ufaransa kuthibitisha matumizi ya kemikali ya Novichok.Ikulu ya rais wa Ufaransa Elysee, imesema katika taarifa kuwa Macron alimwambia Putin kwa njia ya simu kwamba ni muhimu aeleze anayoyajua bila kuchelewa kuhusu tukio hilo la jaribio la mauaji ya mwanasiasa huyo wa upinzani.Macron pia alimfahamisha Putin kuwa uchunguzi wao umethibitisha kama ule uliofanywa na Ujerumani kuwa Navalny alipewa sumu aina ya Novichok, hatua ambayo ni kinyume na kanuni za kimataifa za kutumia silaha za kemikali.,

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amemtolea wito mwenzake wa Urusi Vladimir Putin kutoa ufafanuzi haraka juu ya jaribio la mauaji dhidi ya mwanasiasa wa upinzani Alexei Navalny baada ya uchunguzi uliofanywa na Ufaransa kuthibitisha matumizi ya kemikali ya Novichok.

Ikulu ya rais wa Ufaransa Elysee, imesema katika taarifa kuwa Macron alimwambia Putin kwa njia ya simu kwamba ni muhimu aeleze anayoyajua bila kuchelewa kuhusu tukio hilo la jaribio la mauaji ya mwanasiasa huyo wa upinzani.

Macron pia alimfahamisha Putin kuwa uchunguzi wao umethibitisha kama ule uliofanywa na Ujerumani kuwa Navalny alipewa sumu aina ya Novichok, hatua ambayo ni kinyume na kanuni za kimataifa za kutumia silaha za kemikali.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *