Macron ahimiza uungwaji mkono kwa Lebanon katikati ya mizozo, noreply@blogger.com (Muungwana Blog 2), on September 1, 2020 at 6:00 pm

September 1, 2020

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amesema taifa lake litasimama na Lebanon na watu wake wakati wa kipindi hiki cha mzozo.Amesema hayo wakati wa ziara yake kwenye taifa hilo la Mashariki ya Kati. Macron ameandika kwenye ukurasa wake wa twitter baada ya kupanda mti kwenye eneo la pori kaskazini mwa Beirut kuadhimisha miaka 100 ya uhuru wa taifa hilo.Amesema Lebanon inaweza kuzaliwa upya. Macron, ambaye anafanya ziara ya pili nchini Lebanon tangu mripuko mbaya wa Agosti 4 katika mji mkuu wa Beirut pia ametembelea eneo kulikotokea mripuko huo na kukutana na wawakilishi wa mashirika ya misaada ya kiutu.Mchana huu amekutana na rais Michel Aoun na kuongeza shinikizo la mageuzi katika taifa hilo linaloporomoka kutokana na mzozo wa kiuchumi.Macron ameonya wanasiasa kutoweka mazingira hatari ya vikwazo iwapo watashindwa kulipeleka taifa hilo kwenye mkondo mpya katika kipindi cha miezi mitatu.,

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amesema taifa lake litasimama na Lebanon na watu wake wakati wa kipindi hiki cha mzozo.

Amesema hayo wakati wa ziara yake kwenye taifa hilo la Mashariki ya Kati. Macron ameandika kwenye ukurasa wake wa twitter baada ya kupanda mti kwenye eneo la pori kaskazini mwa Beirut kuadhimisha miaka 100 ya uhuru wa taifa hilo.

Amesema Lebanon inaweza kuzaliwa upya. Macron, ambaye anafanya ziara ya pili nchini Lebanon tangu mripuko mbaya wa Agosti 4 katika mji mkuu wa Beirut pia ametembelea eneo kulikotokea mripuko huo na kukutana na wawakilishi wa mashirika ya misaada ya kiutu.

Mchana huu amekutana na rais Michel Aoun na kuongeza shinikizo la mageuzi katika taifa hilo linaloporomoka kutokana na mzozo wa kiuchumi.

Macron ameonya wanasiasa kutoweka mazingira hatari ya vikwazo iwapo watashindwa kulipeleka taifa hilo kwenye mkondo mpya katika kipindi cha miezi mitatu.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *