Machuma: Acheni kuchagua viongozi kwa kuangalia itikadi au ukabila, on September 10, 2020 at 10:00 am

September 10, 2020

Na Hamisi Nasri, Masasi    WANANCHI wa jimbo la Masasi mjini,mkoani Mtwara wameshauriwa kuacha utamaduni wa kupenda kuchagua viongozi kwa kuangalia itikadi ya ukabila badala yake wachaguwe kwa kuzingatia sifa bora za kiongozi ikiwemo kuthamini wananchi wake.   Kauli hiyo ilitolewa jana mjini Masasi na mgombea ubunge wa jimbo la Masasi mjini kwa chama cha wananchi (CUF) Hamza Machuma alipokuwa akiwabutubia mamia ya wananchi wilaya ya Masasi kwenye mkutano wa kampeni za mgombea huyo pamoja na madiwani wa chama hicho, mkutano ambao ulifanyika katika viwanja vya Mti Mwiba mjini Masasi.   Alisema jimbo la Masasi mjini kumekuwa na desturi kwa baadhi ya wananchi kuchagua viongozi kwa kuangalia itikadi zao za ukabila badala ya kuchagua kiongozi kwa kuangalia sifa bora za kiongozi.  Machuma alisema hakuna jambo baya kama kuchagua kiongozi kwa kuangalia ukabila wake kwani kuna uwezekano mkubwa wa kupata kiongozi ambaye hana uwezo wa kiutendaji hivyo itakuwa ngumu kwa kiongozi huyo kuweza kusukuma maendeleo kwa wananchi.  Mimi wakati nafikirikia kugombea nafasi hii wapo walionifuata na kuniambia wewe ni mmakonde huwezi kupata ubunge kwani katika jimbo hili wamakonde haweze kupata ubunge sasa nisema mimi nitapata ubunge hata kama ni mmakonde na sito hapa hapa Masasi,”alisema Machuma.   Alisema suala la ukabila lisiwagawe wananchi katika uchaguzi na kupelekea ifikapo oktoba 28 mwaka huu kuchagua kiongozi kwa kigezo hicho kiongozi bora hapatikani kwa ajili ya kabila lake.   Aidha,Machuma alisema iwapo wananchi hao wakimchagua kuwa mbunge wa jimbo hilo anaahidi kununua basi maalumu ambao litatumika kwa ajili ya kubeba wananfunzi na kuwapelekea shuleni kila siku za masomo.   Alisema kipaumbele chake kingine ambacho atakitekeleza akiwa mbunge ni suala la kilimo hasa korosho, mbaazi,choroko na Mahindi kuweza kuwa mazao yenye tija kwa wakulima tofauti na ilivyo hivi sasa.   Naye mjumbe wa halmashauri kuu ya chama cha wananchi (CUF) Walindi Shaibu alisema chama cha CUF kimejipanga kushinda majimbo yaote 10 ya mkoa wa Mtwara kwa vile sera zake zina malengo chanya kwa wananchi wa mkoa huo.   Alisema hakuna njia nyingine sahihi ya kuitoa CCM madarakani isipokuwa ni siku ya tarehe 28 oktoba kujitokeza kwa wingi na kupiga kura kwa kuichagua CUF kwa kishindo.,

Na Hamisi Nasri, Masasi  

 

 WANANCHI wa jimbo la Masasi mjini,mkoani Mtwara wameshauriwa kuacha utamaduni wa kupenda kuchagua viongozi kwa kuangalia itikadi ya ukabila badala yake wachaguwe kwa kuzingatia sifa bora za kiongozi ikiwemo kuthamini wananchi wake.

   Kauli hiyo ilitolewa jana mjini Masasi na mgombea ubunge wa jimbo la Masasi mjini kwa chama cha wananchi (CUF) Hamza Machuma alipokuwa akiwabutubia mamia ya wananchi wilaya ya Masasi kwenye mkutano wa kampeni za mgombea huyo pamoja na madiwani wa chama hicho, mkutano ambao ulifanyika katika viwanja vya Mti Mwiba mjini Masasi.

   Alisema jimbo la Masasi mjini kumekuwa na desturi kwa baadhi ya wananchi kuchagua viongozi kwa kuangalia itikadi zao za ukabila badala ya kuchagua kiongozi kwa kuangalia sifa bora za kiongozi.

  Machuma alisema hakuna jambo baya kama kuchagua kiongozi kwa kuangalia ukabila wake kwani kuna uwezekano mkubwa wa kupata kiongozi ambaye hana uwezo wa kiutendaji hivyo itakuwa ngumu kwa kiongozi huyo kuweza kusukuma maendeleo kwa wananchi.

  Mimi wakati nafikirikia kugombea nafasi hii wapo walionifuata na kuniambia wewe ni mmakonde huwezi kupata ubunge kwani katika jimbo hili wamakonde haweze kupata ubunge sasa nisema mimi nitapata ubunge hata kama ni mmakonde na sito hapa hapa Masasi,”alisema Machuma.

   Alisema suala la ukabila lisiwagawe wananchi katika uchaguzi na kupelekea ifikapo oktoba 28 mwaka huu kuchagua kiongozi kwa kigezo hicho kiongozi bora hapatikani kwa ajili ya kabila lake.

   Aidha,Machuma alisema iwapo wananchi hao wakimchagua kuwa mbunge wa jimbo hilo anaahidi kununua basi maalumu ambao litatumika kwa ajili ya kubeba wananfunzi na kuwapelekea shuleni kila siku za masomo.

   Alisema kipaumbele chake kingine ambacho atakitekeleza akiwa mbunge ni suala la kilimo hasa korosho, mbaazi,choroko na Mahindi kuweza kuwa mazao yenye tija kwa wakulima tofauti na ilivyo hivi sasa.

   Naye mjumbe wa halmashauri kuu ya chama cha wananchi (CUF) Walindi Shaibu alisema chama cha CUF kimejipanga kushinda majimbo yaote 10 ya mkoa wa Mtwara kwa vile sera zake zina malengo chanya kwa wananchi wa mkoa huo.

   Alisema hakuna njia nyingine sahihi ya kuitoa CCM madarakani isipokuwa ni siku ya tarehe 28 oktoba kujitokeza kwa wingi na kupiga kura kwa kuichagua CUF kwa kishindo.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *