Maandamano ya kumpinga Netanyahu yaendelea huko Israel,

October 4, 2020

 

Maandamano yanaendelea huko Israeli, yakimtaka Waziri Mkuu Benyamin Netanyahu ajiuzulu kwa sababu ya kushindwa kupambana na janga la corona.

Kulingana na habari iliyochapishwa kwenye wavuti ya gazeti la Yediot Ahronot, makumi ya maelfu ya watu wamefanya maandamano jana katika miji tofauti, ukiwemo mji mkuu wa Tel Aviv, wakitaka Netanyahu ajiuzulu.

Polisi wa Israel, ambao waliingilia kati katika maandamano hayo, waliwashikilia wanaharakati 13 katika miji ya Tel Aviv na Kfar Saba na kumfunga mwandamizi mmoja wa kike.

Katika mji wa Haifa, wafuasi wa Netanyahu walijibu maandamano hayo kwa kuwatupia fataki waandamanaji.

Kulingana na habari katika kituo cha televisheni cha  Channel 12, imebainika kuwa waandamanaji walizingatia kutokwenda mbali sana na makazi yao kutokana na sheria ya kukaa karantini.

Nchi ya Israeli, ambayo imeathiriwa na wimbi la pili la Covid-19 na ambapo ukosefu wa ajira umezidi asilimia 20, imekumbwa na maandamano makubwa dhidi ya Netanyahu kwa zaidi ya miezi 4 kwa sababu ya “usimamizi mbaya wa mchakato dhidi ya janga la corona ” na kesi ya ufisadi inayomkabili.

Mnamo Septemba 18, Utawala wa Israel ulifanya uamuzi wa kuwarudisha watu karantini ya wiki 3 ili kudhibiti mlipuko wa Covid-19.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *