Maandamano makubwa Nigeria dhidi ya ukatili wa polisi,

October 18, 2020

 

Raia wa Nigeria walimiminika katika barabara za mji mkuu wa nchi hiyo Lagos jana kujiunga katika shinikizo zinazoongezeka dhidi ya ukatili wa polisi .

Zaidi ya waandamanaji elfu 10 walifanya maandamano na kufunga barabara na kusababisha kusitishwa kwa biashara katika kituo hicho cha kibiashara .

Ghadhabu dhidi ya kitengo maalumu cha polisi cha kukabiliana na wizi SARS iliibuka kuwa maandamano makubwa wiki iliyopita na kuilazimu serikali ya nchi hiyo kuvunjilia mbali kitengo hicho. 

Waandamanaji hao wameendelea kuandamana licha ya tangazo la marekebisho kadhaa kutoka kwa mamlaka nchini humo.

Wimbi hilo la maandamano ndilo kubwa zaidi la dhihirisho la ushawishi wa watu katika muda wa miaka kadhaa katika taifa hilo lenye idadi kubwa ya watu barani Afrika huku vijana wakitaka mabadiliko kadhaa kufanyika. 

Mamlaka nchini Nigeria imebuni kitengo cha SWAT kuchukuwa mahala pa SARS na kuahidi kuwachukulia hatua maafisa waliohusika katika ukiukaji wa haki.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *