Maandamano dhidi ya serikali yaendelea Thailand,

October 18, 2020

Maandamano yameendelea kufanyika kwa ajili ya kupiga serikali ya Thailand kwa mageuzi ya katiba na kumtaka Waziri Mkuu Prayut Chan-ocha kujiuzulu.

Waandamanaji waliendeleza maandamano hayo kwa siku ya nne licha ya serikali kuweka marufuku ya mikusanyiko na kutangaza ilani ya hali ya dharura nchini Thailand.

Waandamanaji hao walikusanyika kwenye maeneo mbalimbali ya mji mkuu wa Bangkok na kutoa kaulimbiu za kuitaka serikali nzima kujiuzulu huku wakitoa wito wa marekebisho ya mfumo wa sera za kijeshi na utawala wa kifalme.

Huduma za usafiri ziliweza kusitishwa kwenye vituo vitatu vya treni za mwendokasi baada ya watu kukusanyika kufuatia wito uliotolewa mida ya mchana na waandamanaji kupitia mtandao wa kijamii.

Katika mkutano wa baraza la mawaziri uliofanyika hapo jana, Waziri Mkuu Prayut alitangaza kuwa atachukuwa hatua ya kuweka marufuku ya kutoka nje nchini nzima endapo maandamano yaliyoanzishwa miezi miwili iliyopita yataendelea.

Wapinzani wa serikali walianzisha maandamano mnamo tarehe 14 Desemba mwaka jana baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2019 kufanyika ambapo serikali ilikifunga chama cha upinzani cha Future Forward Party na kufukuza viongozi wake bungeni.

Watu wapatao 50,000 walikushiriki maandamano ya wapinzani yaliyofanyika katika mji mkuu wa Bangkok tarehe 19 Septemba na kuendeleza hadi tarehe 14 na 15 Oktoba.

Mara ya mwisho serikali ilitangaza ilani ya hali ya dharura tarehe 15 Oktoba mjini Bangkok , na kuweka marufuku ya mikusanyiko ya watu zaidi ya 5.

Siku hiyo hiyo, waandamanaji hawakuzingatia uamuzi huo wa serikali na badala yake, wakaamua kukusanyika ili kuendeleza maandamano mjini Bangkok.

 

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *