Maalim Seif Atakiwa Kufika Mbele ya Kamati ya Maadili Leo

October 15, 2020

 

Mgombea wa Urais wa #Zanzibar kupitia ACT-Wazalendo, Maalim Seif ametakiwa kufika mbele ya Kamati ya Maadili ya Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) kwa tuhuma za kukiuka Maadili ya Uchaguzi zilizowasilishwa na Chama cha Demokrasia Makini

Seif ameitwa na Kamati hiyo kutokana na kauli aliyoitoa siku za hivi karibuni ya kuwaambia watu wakapige kura Oktoba 27 mwaka huu badala ya Octoba 28, siku iliopangwa na ZEC

Malalamiko hayo dhidi ya Maalim Seif yanatarajiwa kusikilizwa na kutolewa uamuzi leo.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *