Maalim Seif aahidi kurejesha haya zanzibar,

October 13, 2020

 

Mgombea Urais Zanzibar, kwa tiketi ya chama cha Act-Wazalendo Maalim Seif Hamad,amesema kama wananchi watampa ridhaa ya kuiongoza Zanzibar atahakikisha wanapata haki ya kufanya maamuzi wao wenyewe.

Akizungumza leo, katika muendelezo wa  kampeni zake zilizofanyika Jadida Pemba,mgombea huyo ameahidi kurejesha mamlaka kamili ya wazanzibari ili waweze kufanya wanayoyataka.

”Tukiwa na mamlaka yetu kamili tutafanya mambo yetu yote tunayoyataka wala tabia ya maamuzi  kutolewa Dodoma tarehe 29 ndio mwisho” amesema Maalim Seif

Aidha mgombea huyo amewataka vijana pamoja na wananchi wote kwa ujumla kumchagua ili waweze kudai haki ya nchi yao.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *