Maalim Seif Aahidi kuifanya Zanzibar kuwa kitovu cha uchumi barani Afrika., on September 21, 2020 at 8:09 am

September 21, 2020

Mgombea urais wa Zanzibar kupitia tiketi ya ACT- Wazalendo, Maalim Seif Sharif Hamad, amesema anakusudia kuifanya Zanzibar kuwa kitovu cha uchumi barani Afrika.Maalim aliyaeleza hayo katika mkutano wake wa kampeni uliofanyika viwanja vya Alabama Michenzani Wilaya ya Mjini Unguja.Maalim Seif alisema anakusudia kuifanya Zanzibar kuwa na bandari, ambayo wafanyabiashara wataweza kuingiza bidhaa zao bila ya ushuru na wakati wa kutoa watatozwa ushuru kidogo sana.Alisema akilifanya hilo, wafanyabiashara wa nchi za Afrika Mashariki na Kati wataweza kuingia Zanzibar na kujipatia bidhaa zote wanazozitaka na ushuru utakuwa mdogo.Maalim Seif kadhalika aliweka wazi kuwa katika miaka yake mitano atahakikisha Zanzibar inakuwa na shirika lake la ndege ambalo ndege zake zitatembea duniani kote.,

Mgombea urais wa Zanzibar kupitia tiketi ya ACT- Wazalendo, Maalim Seif Sharif Hamad, amesema anakusudia kuifanya Zanzibar kuwa kitovu cha uchumi barani Afrika.

Maalim aliyaeleza hayo katika mkutano wake wa kampeni uliofanyika viwanja vya Alabama Michenzani Wilaya ya Mjini Unguja.

Maalim Seif alisema anakusudia kuifanya Zanzibar kuwa na bandari, ambayo wafanyabiashara wataweza kuingiza bidhaa zao bila ya ushuru na wakati wa kutoa watatozwa ushuru kidogo sana.

Alisema akilifanya hilo, wafanyabiashara wa nchi za Afrika Mashariki na Kati wataweza kuingia Zanzibar na kujipatia bidhaa zote wanazozitaka na ushuru utakuwa mdogo.

Maalim Seif kadhalika aliweka wazi kuwa katika miaka yake mitano atahakikisha Zanzibar inakuwa na shirika lake la ndege ambalo ndege zake zitatembea duniani kote.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *