Maalim asimamishwa kufanya kampeni za urais Zanzibar

October 16, 2020

 

Mgombea urais wa chama cha ACT Wazalendo kwa upande wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad amesimamishwa kufanya kampeni na Kamati ya maadili ya Tume ya Uchaguzi Zanzibar- ZEC kwa muda 5.

Adhabu hiyo imetolewa hii leo baada ya kamati hiyo kukaa na kusikiliza malalamiko yaliyo wasilishwa na Chama cha Demokrasia Makini ambapo imemtuhumu mwanasiasa huyo mkongwe kwa kuhamasisha watu kujitokeza na kupiga kura tarehe 27 ambayo kwa mujibu wa sheria imetengwa kwa watu maalumu.

ACT Wazalendo kimeituhumu Tume ya uchaguziya Zanzibar kwa kuwa na upendeleo. Akizungumza na BBC Afisa wa habari na uenezi- Salim Bimani amesema:

‘’Tume ya uchaguzi wa Zanzibar ZEC inatumika na inatumika vibaya dhidi ya chama cha ACT Wazalendo, tuna ushahidi kwasababu masuala mengi ambayo tumekuwa tukiyadai, tukiyaeleza na kuyalalamikia tume hata siku moja haijapata kujibu, hauijapata kutekeleza, taijapata kuwa wazi, kile kinachotakikana kwenye CCM ndicho wanachokifanya.

Kuna mifano mingi kabisa kaa ZEC imekuwa ikibeba upande mmojana huu ndio ushahidi wa wazi.’’

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *