Maafisa wa Marekani wadai kushinikizwa kuficha ukweli wa repoti za ujasusi kuhusu Urusi

September 10, 2020

Dakika 2 zilizopita

Mfichuzi huyo anasema kwamba Chad Wolf kushoto alimwambia kuwacha kutoa uchambuzi kuhusu uingiliaji wa Urusi

Maelezo ya picha,

Mfichuzi huyo anasema kwamba Chad Wolf kushoto alimwambia kuwacha kutoa uchambuzi kuhusu uingiliaji wa Urusi

Afisa wa ngazi ya juu wa ujasusi katika wizara ya usalama wa ndani ya Marekani, amesema kuwa alishinikizwa na uongozi wa shirika la ujasusi kuficha tishio la Urusi la kuingilia uchaguzi kwasababu lingemfanya ”rais aonekane vibaya” .

Mlalamishi aliyefichua taarifa hii, Brian Murphy alisema kuwa alishushwa cheo kwa kukataa kuzifanyia marekebisho ripoti juu ya suala hili na masuala mengine, ikiwa ni pamoja na suala la utawala wa wazungu.

Maagizo aliyopewa yalikuwa ni kinyume cha sheria, alidai.

Ikulu ya White House na Wizara ya usalama ya ndani imekanusha madai hayo. Mlalamishi aliachiliwa na kamati ya ujasusi ya bunge baadaye mwezi huu.

Ni tuhuma zipi zinazoihusisha Urusi?

Mfichuzi amabaye ni mlalamikaji, Jumanne alitoa madai kadhaa dhidi ya Waziri wa zamani wa wizara ya usalama wa ndani ya Marekani Kirstjen Nielsen, ambaye kwa sasa ni kaimu waziri wa Chad Wolf na naibu wake Ken Cuccinelli.

Bwana Murphy alisema kwamba, kati ya mwezi Machi 2018 na Agosti 2020, kulikuwa na ”matukio yaliyorudiwa ya matumizi mabaya ya mamlaka” kujaribu kuzuwia uchambuzi wa taarifa za kijasusi na utawala usiofaa wa mpango wa ujasusi unaohusiana na juhudi za Urusi za kushawishi na kudhoofisha maslahi ya Marekani “.

Katikati ya mwezi Mei 2020, aliagizwa na Wolf “kuacha kutoa tathmini ya kijasusi juu ya tishio la uingiliaji wa Urusi…na badala yake kuanza kuripoti juu ya shughuli za uingiliaji wa Uchina na Iran “. Maagizo haya yalitolewa moja kwa moja kutoka kwa mshauri wa White House wa masuala ya usalama Robert O’Brien, alisema mlalamikaji.

Bwana Murphy alikataa kuonyesha ushirikiano wa maagizo hayo “kwasababu kufanya hivyo kungeliweka taifa katika hatari ” lakini, mwezi Julai, aliambiwa kuwa ripoti ya ujasusi inapaswa “kuzuiwa” kwasababu ”ingemfanya rais aonekane vibaya”.

Mlalamikaji alisema kuwa Bwana Murphy wakati huo aliondolewa katika mikutano na mwezi Julai alishushwa cheo kutoka kaimu waziri na katibu mkuu wa wizara hadi kuwa msaidizi wa naibu waziri katika kitengo cha utawala. Anataka arejeshwe tena katika cheo chake.

Rais Trump amepinga madai kwamba Urusi iliingilia katika uchaguzi wa mwaka 2016, licha ya matokeo ya uchunguzi wa idara ya ujasusi ya Marekani kubaini kuwa Urusi iliingilia, na aliyataja madai hayo kuwa ”utapeli ‘ wenye uchochezi wa kisiasa.

Ni madai yapi mengine yaliyotolewa?

Bwnaa Murphy anadai alikuwa anakabiliwa na shinikizo kutoka kwa White House la kumtaka atie chumvi juu ya idadi ya wahamiaji na uhusiano na ugaidiwakati ambapo utawala ulipokuwa unatekeleza hatua kali za kuzuwia kuingia nchini humo kwa wahamiaji ambao hawakuwa na makaratasi waliokuwa wanafika kwenye mpaka kati ya Marekani na Mexico, na atoe sababu ya kujengwa kwa ukuta.

” Bwana Murphy alikataa kuzuwia au kubadilisha taarifa za kijasusi ,” alisema mlalamikaji.

Mfichuzi huyo alimlaumu Kirstjen Nielsen kwa kutoa ushaidi wa uwongo kwa kamati mbili za bunge

Maelezo ya picha,

Mfichuzi huyo alimlaumu Kirstjen Nielsen kwa kutoa ushaidi wa uwongo kwa kamati mbili za bunge

Mlalamikaji alidai kuwa waziri wa zamani Nielse alitoa “taarifa za uongo” kwa makusudi juu ya magaidi wanaofahamika na wasiofahamika waliokamatwa kwenye mpaka wakati wa vikao vya kamati za bunge , mwezi Disemba 2018 na mwezi Machi 2019.

Alisema kuwa ushahidi wa Bi Nielsen mwezi Machi 2019 ulijumuisha idadi isiyo sahihi na “ulijumuisha kwa makusudi na taarifa za gushi”. Bi Nielson alijiuzulu wadhifa huo mwezni mmoja baadae, kufuatia malalamiko kutoka kwa Bwana Trump kwamba hakuwa mkali katika mausla ya uhamiaji.

Malalamiko hayo pia yalielezea kwa kina jinsi alivyolumbana na Bwana Cuccinelli juu ya ripoti mwezi Mei juu ya tisho la makundi ya wazungu wenye itikadi kali, akidai kuwa Bwana Cuccinelli aliagiza kufanyika kwa mabadiliko ”katika ambayo yalifanya tisho hilo kuonekana kuwa ni dogo”.

Bwnaa Murphy pia aliagizwa na Bwana Wolf pamoja na Bwana Cuccinelli ku “rekebisha tathmini na ujasusi ” juu ya makundi ya mrengo wa kushoto kama vile antifa “ili kuhakikisha yanawiana na kauloi za umma za Trump”.

Bwana Trump mara kwa mara amekuwa akililaumu kundi la antifa – kwa kusababisha “anti-fascist”, ghasia za mtandao wanaharakati wa mrengo wa kushoto – ambao umekuwa ukitekeleza kwa kiwango kikubwa ghasia ambazo zilizoibuka kote nchini Marekani kufuatia kifo George Floyd kilichojtokea mikononi mwa polisi.

Je madai hayo hamepokelewa vipi ?

Msemaji wa Ikulu ya White House Bi Sarah Matthews alisema: “Balozi O’Brien hajawahi kutaka kushawishi utendaji kazi wa maafisa wa ujasusi juu ya vitisho vya maadili ya uchaguzi wetu au mada nyingine zinazofanyiwa uchunguzi, mambo mengine yanayosemwa na mfanyakazi wa zamani , ambaye hajawahi kukutana nae au kumsikia, ni uongo na ya kumshushia heshima .”

Wizara ya usalama wa ndani pia imepinhga madai hayo, huku msemaji wake Alexei Woltornist akisema: “Tunakanusha kwamba kuna ukweli wowote juu ya madai ya Bwana Murphy”.

Lakini Adam Schiff, mwenyekiti wa kamati ya bunge ya chama cha Democratic ya masuala ya ujasusi alisema : “Tutalichunguza kwa undani hili, tufichue uovu wote au ufisadi kwa watu wa Marekani na tukomesha tabia ya kuuingiza ujasusi katika siasa.”

Source link

,Dakika 2 zilizopita Chanzo cha picha, Reuters Maelezo ya picha, Mfichuzi huyo anasema kwamba Chad Wolf kushoto alimwambia kuwacha kutoa…

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *