Lusinde: Mimi nilikuwa na Lissu Bungeni, hajawahi zungumzia maendeleo ni malalamiko tu na ndiyo maana nilikuwa namuita Malalamiko FC

September 7, 2020

Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Livingstone Lusinde amewaonya wagombea wa vyama vya upinzani waache kutumia muda mwingi kueneza uongo na kumshambulia mgombea wa CCM, John Magufuli.Akizungumza jana na waandishi wa habari jijini Dodoma, Lusinde alimnyoshea kidole mgombea wa urais wa Tanzania kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Tundu Lissu akimweleza kuwa anapaswa kuzungumzia sera na kuwaelezea atawafanyia nini wananchi badala ya kutumia kampeni kumshambulia Magufuli.Alisema ili kuondokana na hali hiyo, katika Bunge lijalo atapendekeza Sheria ya Uchaguzi ibadilishwe ili kuthibiti vyama vinavyoacha kunadi sera na kushambulia wengine.”Haiwezekani kuwa na mtu muda wote analalamika tu, mimi nilikuwa na Lissu (Tundu) bungeni hajawahi zungumzia maendeleo ni malalamiko tu na ndio maana nilikuwa namuita Malalamiko FC, kimekuwa chama cha malalamiko na kuzungumza kashfa na kejeli.” alisema na kuongeza;”Wana bahati mwaka huu Mwenyekiti wetu (Rais Magufuli) ametukataza kuzungumza kashfa wakati wa kampeni. Nilikuwa nimeagiza kontena tatu hivi na zilikuwa zimefika bandarini, shughuli ingekuwa nzito, wamshukuru Rais Magufuli alivyowabeba amekemea hataki kampeni za matusi wala kashfa, lakini tunavumilia inafika mahali tutashindwa.”alisema Lusinde.Alisema Lissu alishambuliwa na linajulikana, ila si sahihi kusema serikali ilihusika na ameliomba Jeshi la Polisi limtafute muhusika ili serikali isiendelee kuchafuliwa.”Pia Lissu amekuwa akiziimba risasi 16 je ndio ilani?, anasema wananchi wanahofu, mbona yeye tangu afike hapa nchini hatujamuona akiwa na barakoa na anatembea kila mahali bila hofu na kwa uhuru, sasa hiyo hofu ya kwa wananchi iko wapi? aache uongo na azungumzie sera kama wanazo,”alisema Lusinde.Alisema Rais Magufuli amejipambanua kuwa ni mwadilifu na mzalendo mwenye lengo la kuifanya Tanzania kupiga hatua za maendeleo huku akifanya kampeni kistaarabu bila kumshambulia mtu na kuomba kura kwa watu wote.”Ameomba kura hadi upinzani wamchague, hajambagua mtu, hajashambulia mtu, muda wote anapambana kuhakikisha anapata ushindi wake na chama chake ili kuendelea kuwatumikia wananchi katika miaka mitano mingine,”alisema.Kuhusu mgombea wa nafasi ya urais wa Tanzania kwa chama cha ACT Wazalendo, Bernad Membe mgombea Lusinde alimshangaa kuendelea kupiga kampeni muda mrefu katika mkoa mmoja na kusema wagombea kama hao wanapoteza muda na kuitia nchi hasara.”Wakati mgombea wa CCM, Rais John Magufuli akiwa amefikisha mikoa tisa kwenye kampeni zake na kukanyanga kiatu kweli kweli, mgombea wa ACT-Wazalendo bado yuko Lindi, sijui anagombea urais wa Lindi au wa kijiji cha Londo, baadaye hawa wagombea watapiga kelele kuwa wameibiwa kura, nataka Watanzania walione hili mapema.”alisema Lusinde.Alisema Mkoa wa Dodoma umeamua kura zote apewe Rais Magufuli kutokana na kuibadilisha sana jiji hilo. “Tunataka kuvunja rekodi ya kumpa ushindi wa kishindo Magufuli ili awe na deni kwa Watanzania litakalomfanya apige kazi kwa kiwango cha kutisha nchi isonge mbele. Magufuli sio mtu wa kusafiri nje ya nchi, lakini ameweza kuibadili nchi kwa kiwango kikubwa na kuifanya maeneo mengi yanafanana na nchi za nje.”alisema.,

Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Livingstone Lusinde amewaonya wagombea wa vyama vya upinzani waache kutumia muda mwingi kueneza uongo na kumshambulia mgombea wa CCM, John Magufuli.

Akizungumza jana na waandishi wa habari jijini Dodoma, Lusinde alimnyoshea kidole mgombea wa urais wa Tanzania kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Tundu Lissu akimweleza kuwa anapaswa kuzungumzia sera na kuwaelezea atawafanyia nini wananchi badala ya kutumia kampeni kumshambulia Magufuli.

Alisema ili kuondokana na hali hiyo, katika Bunge lijalo atapendekeza Sheria ya Uchaguzi ibadilishwe ili kuthibiti vyama vinavyoacha kunadi sera na kushambulia wengine.

“Haiwezekani kuwa na mtu muda wote analalamika tu, mimi nilikuwa na Lissu (Tundu) bungeni hajawahi zungumzia maendeleo ni malalamiko tu na ndio maana nilikuwa namuita Malalamiko FC, kimekuwa chama cha malalamiko na kuzungumza kashfa na kejeli.” alisema na kuongeza;

“Wana bahati mwaka huu Mwenyekiti wetu (Rais Magufuli) ametukataza kuzungumza kashfa wakati wa kampeni. Nilikuwa nimeagiza kontena tatu hivi na zilikuwa zimefika bandarini, shughuli ingekuwa nzito, wamshukuru Rais Magufuli alivyowabeba amekemea hataki kampeni za matusi wala kashfa, lakini tunavumilia inafika mahali tutashindwa.”alisema Lusinde.

Alisema Lissu alishambuliwa na linajulikana, ila si sahihi kusema serikali ilihusika na ameliomba Jeshi la Polisi limtafute muhusika ili serikali isiendelee kuchafuliwa.

“Pia Lissu amekuwa akiziimba risasi 16 je ndio ilani?, anasema wananchi wanahofu, mbona yeye tangu afike hapa nchini hatujamuona akiwa na barakoa na anatembea kila mahali bila hofu na kwa uhuru, sasa hiyo hofu ya kwa wananchi iko wapi? aache uongo na azungumzie sera kama wanazo,”alisema Lusinde.

Alisema Rais Magufuli amejipambanua kuwa ni mwadilifu na mzalendo mwenye lengo la kuifanya Tanzania kupiga hatua za maendeleo huku akifanya kampeni kistaarabu bila kumshambulia mtu na kuomba kura kwa watu wote.

“Ameomba kura hadi upinzani wamchague, hajambagua mtu, hajashambulia mtu, muda wote anapambana kuhakikisha anapata ushindi wake na chama chake ili kuendelea kuwatumikia wananchi katika miaka mitano mingine,”alisema.

Kuhusu mgombea wa nafasi ya urais wa Tanzania kwa chama cha ACT Wazalendo, Bernad Membe mgombea Lusinde alimshangaa kuendelea kupiga kampeni muda mrefu katika mkoa mmoja na kusema wagombea kama hao wanapoteza muda na kuitia nchi hasara.

“Wakati mgombea wa CCM, Rais John Magufuli akiwa amefikisha mikoa tisa kwenye kampeni zake na kukanyanga kiatu kweli kweli, mgombea wa ACT-Wazalendo bado yuko Lindi, sijui anagombea urais wa Lindi au wa kijiji cha Londo, baadaye hawa wagombea watapiga kelele kuwa wameibiwa kura, nataka Watanzania walione hili mapema.”alisema Lusinde.

Alisema Mkoa wa Dodoma umeamua kura zote apewe Rais Magufuli kutokana na kuibadilisha sana jiji hilo. “Tunataka kuvunja rekodi ya kumpa ushindi wa kishindo Magufuli ili awe na deni kwa Watanzania litakalomfanya apige kazi kwa kiwango cha kutisha nchi isonge mbele. Magufuli sio mtu wa kusafiri nje ya nchi, lakini ameweza kuibadili nchi kwa kiwango kikubwa na kuifanya maeneo mengi yanafanana na nchi za nje.”alisema.,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *