Lulu Diva Asimulia Alivyonusa Kifo!

September 19, 2020

Sexy lady kunako Bongo Flevani, Lulu Abbas ‘Lulu Diva’ amesimulia alivyonusa kifo laivu.Katika mahojiano maalum, Lulu Diva ameliambia Gazeti la IJUMAA kuwa, hadi sasa amekuwa akilikumbuka tukio la wiki iliyopita alipokutana uso kwa uso na Iziraili Mtoa-Roho za watu katika ajali mbaya aliyoipata maeneo ya Chalinze mkoani Pwani akiwa na wasanii wenzake, Belle 9 na Bonge la Nyau walipokuwa wakirejea jijini Dar wakitokea kwenye shoo za kampeni mkoani Iringa.Lulu Diva amesema kuwa, wakati wanakutana na balaa hilo alikuwa amesinzia hivyo hakujua ni nini hasa kilichotokea.Alisema, alishtushwa na mlio mkubwa kiasi kwamba aliona wazi huo ndiyo ulikuwa mwisho wa maisha yake na kuona kuwa kilichobaki ilikuwa ni kusali tu ili kujikabidhi kwa Muumba wa mbingu na ardhi.“Kiukweli ajali mtu aisikie tu kwa mwingine kwa sababu mimi nilikiona kifo changu laivu.“Nakumbuka nilikuwa nimelala, lakini nilishtushwa na mlio mkubwa wakati gari linapinduka na hapohapo nilianza kujisomea dua, maana nilikuwa nikiwaangali wezangu nao walikuwa hawajitambui,” anasema Lulu Diva.Mrembo huyo aliendelea kusimulia kuwa, baada ya kuona hali ile hali na kuomba dua, alipoteza fahamu ambapo baadaye alijikuta hospitalini akiwa na jeraha kichwani huku Bonge la Nyau na Belle 9 nao wakiwa na majeraha sehemu za mikononi na kichwani.“Kwenye ajali ile ni Mungu tu aliamua kutupa nafasi nyingine kwa sababu tungeweza kupoteza maisha wote. “Kusema kweli kwenye tukio lile, Mungu alitaka kutufundisha kitu na kweli tumefundishwa kitu,” anasema Lulu Diva ambaye kwa sasa, yeye na wenzake wanaendelea vizuri.,

Sexy lady kunako Bongo Flevani, Lulu Abbas ‘Lulu Diva’ amesimulia alivyonusa kifo laivu.Katika mahojiano maalum, Lulu Diva ameliambia Gazeti la IJUMAA kuwa, hadi sasa amekuwa akilikumbuka tukio la wiki iliyopita alipokutana uso kwa uso na Iziraili Mtoa-Roho za watu katika ajali mbaya aliyoipata maeneo ya Chalinze mkoani Pwani akiwa na wasanii wenzake, Belle 9 na Bonge la Nyau walipokuwa wakirejea jijini Dar wakitokea kwenye shoo za kampeni mkoani Iringa.

Lulu Diva amesema kuwa, wakati wanakutana na balaa hilo alikuwa amesinzia hivyo hakujua ni nini hasa kilichotokea.

Alisema, alishtushwa na mlio mkubwa kiasi kwamba aliona wazi huo ndiyo ulikuwa mwisho wa maisha yake na kuona kuwa kilichobaki ilikuwa ni kusali tu ili kujikabidhi kwa Muumba wa mbingu na ardhi.“Kiukweli ajali mtu aisikie tu kwa mwingine kwa sababu mimi nilikiona kifo changu laivu.

“Nakumbuka nilikuwa nimelala, lakini nilishtushwa na mlio mkubwa wakati gari linapinduka na hapohapo nilianza kujisomea dua, maana nilikuwa nikiwaangali wezangu nao walikuwa hawajitambui,” anasema Lulu Diva.

Mrembo huyo aliendelea kusimulia kuwa, baada ya kuona hali ile hali na kuomba dua, alipoteza fahamu ambapo baadaye alijikuta hospitalini akiwa na jeraha kichwani huku Bonge la Nyau na Belle 9 nao wakiwa na majeraha sehemu za mikononi na kichwani.

“Kwenye ajali ile ni Mungu tu aliamua kutupa nafasi nyingine kwa sababu tungeweza kupoteza maisha wote. “Kusema kweli kwenye tukio lile, Mungu alitaka kutufundisha kitu na kweli tumefundishwa kitu,” anasema Lulu Diva ambaye kwa sasa, yeye na wenzake wanaendelea vizuri.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *