Lionel Messi ashinda kesi ya kutumia nembo ya jina lake

September 17, 2020

Dakika 14 zilizopita

lionel messi in friendly against Girona Sept 16 2020

Lionel Messi sasa anaweza kusajili jina lake kama nembo baada kushinda mzozo wa kisheria wa miaka tisa, mahakama ya juu barani Ulaya imeamua.

Mahakama ya haki ya Ulaya imetupilia mbali rufaa ya ya kampuni ya ya baisikeli ya Massi Uhispania na ofisi ya haki miliki ya muungano wa Ulaya, EUIPO.

Mchezaji soka huyo wa Barcelona alitoa ombi la kutaka kutumia jina lake kama nembo ya vazi la michezo mwaka 2011.

Lakini Massi alipinga ombi hilo likisema kuwa nembo hizo mbili zinakaribiana na huenda ikaleta mkanganyiko.

Mahakama ya Ulaya ya Haki (ECJ) imesema hadhi ya mchezaji nyota huyo itazingatiwa kutathmini ikiwa watu wataweza kutofautisha nembo hizo mbili.

Kwa kuzingatia hilo, ilidumisha uamuzi uliotolewa 2018 na mahakama ya pamoja ya EU ikisema mchezaji huyo anajulika vyema na kwamba suala la mchanganyiko haliwezi kutokea .

Massi, ambayo inauza baisikeli na vifaa vyake, ilifanikiwa katika hatua y akwanza ya kupinga ombi la mshambuliaji huyo wa Barcelona. Lakini ilishindwa baada ya Lionel Messi kuwasilisha rufaa katika mahakama ya Ulaya, ambayo imetoa uamuzi wa sasa.

Messi, 33, ambaye anavalia jezi nambari 10, ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa soka duniani kwa mara sita mtawalio pia ni mchezaji kandanda anayelipwa fedha nyingi zaidi, kwa mujibu wa jarida la Forbes. Linakadiria kuwa mchezaji huyo alilipwa jumla ya $126m kufikia 2020 (£97m).

Mnamo mwezi Agosti, mchezaji huyo aligongwa vichwa vya habari baada ya kuwasilisha ombi la kutaka kuondokaklabu ya Barcelona .

Source link

,Dakika 14 zilizopita Chanzo cha picha, Getty Images Lionel Messi sasa anaweza kusajili jina lake kama nembo baada kushinda mzozo…

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *