Lionel Messi aanza tena mazoezi Barcelona, on September 8, 2020 at 10:00 am

September 8, 2020

Mchezaji maarufu aliyeifungia Barcelona magoli mengi, Lionel Messi amerejea mazoezini kufuatia kushindwa kwa jaribio lake la kulazimisha kuondoka katika klabu hiyo.Messi, 33, aliwasilisha ombi la uhamisho tarehe 25 Agosti lakini Ijumaa iliyopita alisema kuwa ataendelea kubaki katika klabu hiyo kwasababu “haiwezekani ” kwa timu yoyote kulipia kipengele kinachomruhusu kuondoka.Ni mara ya kwanza kwa Muargentina huyo kufanya mazoezi katika klabu hiyo tangu kuwasili kwa meneja mpya Ronald Koeman.Barcelona inaanza mechi dhidi Villarreal kutoka La Liga tarehe 27 Septemba.Messi alifanya mazoezi peke yake kama alivyofanya Philippe Coutinho, huku wachezaji wenzake wakifanya mazoezi pamoja.Messi alishindwa kuhudhuria kupima Covid-19 na wachezaji wenzake tarehe 30 Agosti na hakuhudhuria mazoezi tangu alipotuma ujumbe akiifahamisha klabu hiyo juu ya nia yake ya kutekeleza kipengele katika mkataba wake ambacho anaamini kitamruhusu kuondoka bila malipo mara moja.Barcelona na La Liga kwa pamoja zinasisitiza kwamba kipengele hicho si halali tena – na kwamba klabu yoyote inayotaka kumnunua itatakiwa kulipia garama ya Euro milioni 700 za kipengele cha kumuachilia.Rais wa La Liga Javier Tebas alisema kuwa katika uzinduzi wa msimu wa La Liga wa 2020-21 Jumatatu “hakuwa na wasiwasi mkubwa kabisa ” kwamba Messi angeliondoka Barcelona msimu huu.”Tunataka Messi awe nasi. Ni mchezaji bora katika historia ya soka na tunataka amalizie mchezo wake katika La Liga,” Tebas alisema.”Amekuwa nasi kwa miaka 20 na tunafarijika sana anaendelea kuwa nasi na haendi katika ligi nyingine .”,

Mchezaji maarufu aliyeifungia Barcelona magoli mengi, Lionel Messi amerejea mazoezini kufuatia kushindwa kwa jaribio lake la kulazimisha kuondoka katika klabu hiyo.

Messi, 33, aliwasilisha ombi la uhamisho tarehe 25 Agosti lakini Ijumaa iliyopita alisema kuwa ataendelea kubaki katika klabu hiyo kwasababu “haiwezekani ” kwa timu yoyote kulipia kipengele kinachomruhusu kuondoka.

Ni mara ya kwanza kwa Muargentina huyo kufanya mazoezi katika klabu hiyo tangu kuwasili kwa meneja mpya Ronald Koeman.

Barcelona inaanza mechi dhidi Villarreal kutoka La Liga tarehe 27 Septemba.

Messi alifanya mazoezi peke yake kama alivyofanya Philippe Coutinho, huku wachezaji wenzake wakifanya mazoezi pamoja.

Messi alishindwa kuhudhuria kupima Covid-19 na wachezaji wenzake tarehe 30 Agosti na hakuhudhuria mazoezi tangu alipotuma ujumbe akiifahamisha klabu hiyo juu ya nia yake ya kutekeleza kipengele katika mkataba wake ambacho anaamini kitamruhusu kuondoka bila malipo mara moja.

Barcelona na La Liga kwa pamoja zinasisitiza kwamba kipengele hicho si halali tena – na kwamba klabu yoyote inayotaka kumnunua itatakiwa kulipia garama ya Euro milioni 700 za kipengele cha kumuachilia.

Rais wa La Liga Javier Tebas alisema kuwa katika uzinduzi wa msimu wa La Liga wa 2020-21 Jumatatu “hakuwa na wasiwasi mkubwa kabisa ” kwamba Messi angeliondoka Barcelona msimu huu.

“Tunataka Messi awe nasi. Ni mchezaji bora katika historia ya soka na tunataka amalizie mchezo wake katika La Liga,” Tebas alisema.

“Amekuwa nasi kwa miaka 20 na tunafarijika sana anaendelea kuwa nasi na haendi katika ligi nyingine .”

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *