Libya yatangaza wakuu wa vyombo vya ulinzi, noreply@blogger.com (Muungwana Blog 2), on August 30, 2020 at 10:00 am

August 30, 2020

Kiongozi wa serikali ya umoja wa kitaifa nchini Libya amemteua waziri mpya wa ulinzi na mkuu wa majeshi, baada ya siku kadhaa za maandamano dhidi ya huduma duni za umma na hali ya maisha.Uamuzi huo umetolewa kufuatia tangazo lililotolewa masaa kadhaa yaliopita na serikali ya Libya inayotambuliwa na Umoja wa Mataifa (GNA) kwamba imemsimamisha kazi waziri wake wa mambo ya ndani, kutokana na wanamgambo wenye silaha kuwashambilia kwa risasi kundi la waliokuwa wakiandamana kwa amani juma lililopita.Waziri Mkuu Fayez al-Sarraj amempandisha cheo naibu na kaimu waziri wa ulinzi Salah Eddine al-Namrush kuwa waziri kamili na pia kumteua Jenerali Mohammad Ali al-Haddad kuwa mkuu wa majeshi.Haddad anatokea Misrata, umbali wa kilometa 200 mashariki mwa Libya, maskani ya kundi la wapiganaji lenye nguvu ambalo lilishiriki mapigano bega kwa bega na serikali hiyo ya umoja wa kitaifa dhidi na jeshi la mbabe wa kivita Khalifa Haftar, ambae alikuwa akifanya jaribio la kuuteka mji wa Tripoli mwaka uliopita.,

Kiongozi wa serikali ya umoja wa kitaifa nchini Libya amemteua waziri mpya wa ulinzi na mkuu wa majeshi, baada ya siku kadhaa za maandamano dhidi ya huduma duni za umma na hali ya maisha.

Uamuzi huo umetolewa kufuatia tangazo lililotolewa masaa kadhaa yaliopita na serikali ya Libya inayotambuliwa na Umoja wa Mataifa (GNA) kwamba imemsimamisha kazi waziri wake wa mambo ya ndani, kutokana na wanamgambo wenye silaha kuwashambilia kwa risasi kundi la waliokuwa wakiandamana kwa amani juma lililopita.

Waziri Mkuu Fayez al-Sarraj amempandisha cheo naibu na kaimu waziri wa ulinzi Salah Eddine al-Namrush kuwa waziri kamili na pia kumteua Jenerali Mohammad Ali al-Haddad kuwa mkuu wa majeshi.

Haddad anatokea Misrata, umbali wa kilometa 200 mashariki mwa Libya, maskani ya kundi la wapiganaji lenye nguvu ambalo lilishiriki mapigano bega kwa bega na serikali hiyo ya umoja wa kitaifa dhidi na jeshi la mbabe wa kivita Khalifa Haftar, ambae alikuwa akifanya jaribio la kuuteka mji wa Tripoli mwaka uliopita.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *