Libya: Mkuu wa serikali inayotambuliwa na UN kujiuzulu

September 17, 2020

”Natangaza nia yangu ya dhati ya kukabidhi hatamu za uongozi kwa baraza la utawala linalofuata, kabla ya mwezi Oktoba kumalizika”, ndivyo  alivyotangaza nia yake waziri mkuu Fayez Serraj katika hotuba kwa taifa lake kupitia televisheni usiku a kuamkia leo. Kiongozi  huyo amesema hali ya kisiasa na kijamii nchini Libya iko katika mivutano mikubwa, na hali hiyo inazitatiza juhudi za kutafuta suluhisho la kisiasa na kuepusha umwagikaji wa damu.

Soma zaidi:Ujerumani yaandaa mkutano wa kilele kutafuta amani ya Libya

Waziri mkuu huyo wa serikali ya mjini Tripoli inayotambuliwa na Umoja wa Mataifa amesema kuwa majadiliano ya hivi karibuni baina ya pande hasimu ambayo yalidhaminiwa na Umoja wa Mataifa, yameifikisha Libya katika kipindi kipya cha maandalizi ya kuziunganisha taasisi za kitaifa, na kusafisha njia kuelekea uchaguzi wa bunge na wa rais.

Muda muafaka wa kufunga virago

Libyen Tripolis Fayez Serraj Einheitsregierung Treffen (picture-alliance/AP Photo/GNA Media)

Kikao cha serikali ya umoja wa kitaifa mjini Tripoli, Libya

Waziri Mkuu Fayez Serraj amesema kuwa ni katika mazingira hayo ya kuelekea uchaguzi,ambapo ananuia kuachia ngazi.

”Na kwa nukta hiyo, natangaza nia yangu ya dhati kukabidhi madaraka kwa utawala unaofuata, katika muda usiozidi mwezi ujao wa Oktoba,” amesema Serraj na kuongeza huwa hadi wakati huo ”naamini kamati ya mazungumzo itakuwa imekamiisha kazi na kuchagua baraza jipya la utawala, na kiongozi mpya wa serikali, atakayepokea madaraka. Tunawatakia mafanikio, Mungu akipenda.”

Mkutano mwingine wa kilele kuhusu Libya

Wakati hayo yakiarifiwa, Umoja wa Mataifa kwa ushirikiano na serikali ya Ujerumani inatayarisha mkutano mwingine wa kilele kuhusu Libya, ambao utafanyika kwa njia ya video tarehe tano Oktoba, hilo likiwa ni kwa mujibu wa msemaji wa umoja huo mjini New York.

UN-Generalsekretär Antonio Guterres (Imago Images/Xinhua/)

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres

Katika mkutano huo, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ataungana na mawaziri wa mambo ya nje wa nchi kadhaa, pamoja wa wajumbe wa pande zinazohasimiana nchini Libya.

Hatua nyingine baada ya Berlin

Mkutano huo utakuwa ni mwendelezo wa mwingine uliofanyika mwezi Januari mjini Berlin, ukizishirikisha nchi zote zinazojihusisha katika mzozo wa nchini Libya.

Soma zaidi: Umoja wa Ulaya wataka pande hasimu nchini Libya kuweka silaha chini

Katika mkutano huo, nchi hizo zilikuwa zimeahidi kusimamisha kuyapa silaha makundi yanayopigana vita.

Wawakilishi wa Ujerumani, Umoja wa Mataifa, Marekani, Uingereza, Ufaransa, na China ni miongoni mwa watakaoshiriki katika mkutano huu wa Oktoba. Pande nyingine zitakazokuwa na wajumbe ni Uturuki, Umoja wa Falme za Kiarabu, Jamhuri ya Kongo, Italia, Misri na Algeria. Umoja wa Ulaya, Umoja wa Afrika na Jumuiya ya Nchi za Kiarabu pia watahudhuria mkutano huo.

dpae, afpe

Source link

,”Natangaza nia yangu ya dhati ya kukabidhi hatamu za uongozi kwa baraza la utawala linalofuata, kabla ya mwezi Oktoba kumalizika”,…

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *