Libya kuanza uzalishaji wa mafuta katika viwanja vikubwa vya mafuta nchini humo,

October 11, 2020

Shirika la mafuta la taifa nchini Libya NOC limetangaza leo kuwa linaanza tena shughuli ya uzalishaji mafuta katika eneo kubwa la visima vya mafuta nchini humo huku serikali hasimuupande wa Mashariki na Magharibi nchini humo zikianza mazungumzo ya amani ambayo ni sehemu ya mazungumzo ya kwanza kabla ya mazungumzo yatakayosimamiwa na Umoja wa Mataifa yatakayofanyika mwezi ujao. 

Shirika hilo la NOC limesema kuwa limeondoa marufuku iliyowekwa katika eneo la visima vya mafuta la Sharara baada ya kuafikia makubaliano na vikosi vitiifu kwa kamanda Khalifa Haftar kuondoa vikwazo vyote katika viwanja hivyo. 

Tangazo la shirika hilo linajiri wiki tatu baada ya kamanda Khalifa Haftar aliyekuwa nyuma ya jaribio la mwaka mmoja la kuuteka mji mkuu Tripoli, kutangaza kumalizika kwa vizuizi katika maeneo hayo muhimu kwa taifa hilo.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *