“Kwa Miaka 64 Mume Wangu Alinificha Kuwa ni Usalama wa Taifa”

September 7, 2020

Wanasema Afisa wa Usalama wa Taifa anatakiwa kuwa Mtu mwenye uwezo wa kutunza siri za kazi lakini pia yeye mwenyewe kutojitambulisha au kusema kwa Watu kama anafanya kazi kwenye Idara hiyo nyeti kwenye Taifa lolote.Sasa huko Uingereza Mwanaume mmoja aitwae Glyndwr amejichukulia sifa za kutosha baada ya kufariki ambapo Mjane Audrey Phillips (85) juzi ndio amekuja kujua kwamba Glyndwr ambae ni Mume aliyeishi nae kwa miaka 64, alikua Afisa Usalama wa Taifa huko Uingereza.Amefahamu vipi? …..ni baada ya kifo cha Mume wake huyo ambapo alikua akipanga vitu nyumbani ndipo alipokutana na makaratasi yakionyesha kwamba Glyndwr alikua Afisa Usalama toka akiwa na umri wa miaka 13, Mjane huyu anasema kwa miaka yote ya ndoa alijua Glyndwr alikua Injinia (Mhandisi)Karatasi zilizomfanya atambue kazi aliyokua akiifanya Marehemu Mume wake ni karatasi za siri ambapo Jamaa alikua ameandika historia yake fupi na kuelezea jinsi alivyoanza kuwa Jasusi kwenye miaka ya 1940, Glyndwr alifariki akiwa na umri wa miaka 83.Audrey anasema hakuwahi kushtuka chochote kuhusu hiyo kazi ya Ujasusi ambapo Glyndwr alikua akifanya kazi zake mbali na nyumbani mara nyingi sana, sasa imebidi Mjane huyu aandike kitabu kuhusu maisha yake na ya Marehemu Mume wake na kukipa jina la “Operation XX And Me: Did I have a choice?,

Wanasema Afisa wa Usalama wa Taifa anatakiwa kuwa Mtu mwenye uwezo wa kutunza siri za kazi lakini pia yeye mwenyewe kutojitambulisha au kusema kwa Watu kama anafanya kazi kwenye Idara hiyo nyeti kwenye Taifa lolote.
Sasa huko Uingereza Mwanaume mmoja aitwae Glyndwr amejichukulia sifa za kutosha baada ya kufariki ambapo Mjane Audrey Phillips (85) juzi ndio amekuja kujua kwamba Glyndwr ambae ni Mume aliyeishi nae kwa miaka 64, alikua Afisa Usalama wa Taifa huko Uingereza.
Amefahamu vipi? …..ni baada ya kifo cha Mume wake huyo ambapo alikua akipanga vitu nyumbani ndipo alipokutana na makaratasi yakionyesha kwamba Glyndwr alikua Afisa Usalama toka akiwa na umri wa miaka 13, Mjane huyu anasema kwa miaka yote ya ndoa alijua Glyndwr alikua Injinia (Mhandisi)
Karatasi zilizomfanya atambue kazi aliyokua akiifanya Marehemu Mume wake ni karatasi za siri ambapo Jamaa alikua ameandika historia yake fupi na kuelezea jinsi alivyoanza kuwa Jasusi kwenye miaka ya 1940, Glyndwr alifariki akiwa na umri wa miaka 83.
Audrey anasema hakuwahi kushtuka chochote kuhusu hiyo kazi ya Ujasusi ambapo Glyndwr alikua akifanya kazi zake mbali na nyumbani mara nyingi sana, sasa imebidi Mjane huyu aandike kitabu kuhusu maisha yake na ya Marehemu Mume wake na kukipa jina la “Operation XX And Me: Did I have a choice?

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *