Kwa Mamilioni Haya, Mondi Katoboa, noreply@blogger.com (Udaku Special)

September 2, 2020

NASIBU Abdul almaarufu kama Diamond Platnumz, amekuwa ni nembo ambayo inatangaza vizuri muziki wetu kwa hapa Afrika.Katika burudani, naweza kusema kwa sasa amekuwa ni mwanamuziki ambaye ameliteka sana soko la Bongo Fleva. Wengi waliomtambua na ngoma kama Kamwambie, Mbagala, Lala Salama, Kizaizai, Binadamu na nyingine kibao ambazo zilifanya poa sana na kumtambulisha vizuri.Diamond ambaye ni bosi wa Lebo kubwa ya muziki hapa Bongo ya Wasafi Classic Baby (WCB), ameendelea kuiteka ramani ya muziki wa Bongo Fleva kwa kali za Mondi ambazo zimefanya poa kwa kujikusanyia mamilioni ya watazamaji kwenye mtandao wa YouTube.YOPE REMIXHii ni ngoma ambayo Mondi ameshirikishwa na msanii kutokea Demokrasia ya Kongo, Inno’s B.Yope Remix imetoka miezi kumi na moja iliyopita, lakini imefanya poa sana kwa kutazamwa na watazamaji milioni 109 mpaka sasa na kuvunja rekodi kwa ukanda wa hapa Afrika Mashariki. Japo mwanzo ilitoka original yake na haikufanya vizuri, kama ilivyofanya hii.INAMANi ngoma kali aliyoiachia mnyama Mondi akiwa na mwanamuziki mkali na mwenye vipaji vikali Fally Ipupa. Inama ni ngoma ambayo imetoka mwaka mmoja uliopita na kufanya poa kwenye mtandao wa YouTube kwa kutazamwa na watazamaji milioni 68, kiasi cha kufanya Mondi aonekane bado yuko kileleni.AFRICAN BEAUTYMkwaju mwingine kutoka kwa Mondi wa African Beauty, ambao alivunja rekodi kwa kufanya kolabo na mwanamuziki mkali kutokea nchini Marekani, Omarion.African Beauty tangu imetoka, ni miaka miwili sasa na tayari imejikusanyia kijiji cha watazamaji milioni 51 mpaka sasa na kuendelea kushikilia rekodi ya ngoma kali ambayo bado haijachuja.NANAMkwaju mwingine mkali wa Nana, Mondi akiwa amemshirikisha staa kutokea nchini Nigeria Mr Flavour, umeachiwa miaka mitano iliyopita na kujikusanyia watazamaji milioni 65 mpaka sasa.Ni bonge moja la kolabo ambalo Mondi alilitengeneza akiwa na mwanamuziki huyo mkubwa, ambaye naye anafanya vizuri na ngoma zake hata kwenye chati za muziki.MARRY YOUBado Mondi alitikisa tena kwenye ngoma hii kwa kutengeneza kemistri nyingine akiwa na mwanamuziki mkubwa kutokea nchini Marekani Neyo.Marry You ni ngoma ambayo iliachiwa miaka mitatu iliyopita na kufanya poa kwa kutazamwa zaidi ya mara milioni 44.Kiwango hicho, kimeifanya ngoma ya Marry You kubaki kwenye chati kali, hasa ukiangalia na mwanamuziki aliyeshirikishwa humo.SALOMESalome ni ngoma ya Mondi akiwa na Rayvanny, ambayo nayo ilifanya poa na bado iko kwenye chati. Ngoma hiyo iliachiwa miaka mitatu iliyopita na kutazamwa zaidi ya mara milioni 33 na kuendelea kubaki kwenye ramani nzuri.SIKOMIKatika ngoma za Mondi zilizo na rekodi nzuri ya watazamaji, nayo inaingia. Ni ngoma ambayo iliachiwa rasmi miaka miwili iliyopita na ikafanya poa kwa kutazamwa na watazamaji milioni 44 mpaka sasa.Bado Mondi anaendelea kutikisa na ngoma zake nyingine ambazo zinajizolea watazamaji lukuki kiasi caha kumfanya aendelee kubaki kwenye chati ya wanamuziki wanaofanya poa bara la Afrika na hata kwenye ukanda wa Afrika Mashariki.,

NASIBU Abdul almaarufu kama Diamond Platnumz, amekuwa ni nembo ambayo inatangaza vizuri muziki wetu kwa hapa Afrika.

Katika burudani, naweza kusema kwa sasa amekuwa ni mwanamuziki ambaye ameliteka sana soko la Bongo Fleva. Wengi waliomtambua na ngoma kama Kamwambie, Mbagala, Lala Salama, Kizaizai, Binadamu na nyingine kibao ambazo zilifanya poa sana na kumtambulisha vizuri.

Diamond ambaye ni bosi wa Lebo kubwa ya muziki hapa Bongo ya Wasafi Classic Baby (WCB), ameendelea kuiteka ramani ya muziki wa Bongo Fleva kwa kali za Mondi ambazo zimefanya poa kwa kujikusanyia mamilioni ya watazamaji kwenye mtandao wa YouTube.

YOPE REMIX

Hii ni ngoma ambayo Mondi ameshirikishwa na msanii kutokea Demokrasia ya Kongo, Inno’s B.

Yope Remix imetoka miezi kumi na moja iliyopita, lakini imefanya poa sana kwa kutazamwa na watazamaji milioni 109 mpaka sasa na kuvunja rekodi kwa ukanda wa hapa Afrika Mashariki. Japo mwanzo ilitoka original yake na haikufanya vizuri, kama ilivyofanya hii.

INAMA

Ni ngoma kali aliyoiachia mnyama Mondi akiwa na mwanamuziki mkali na mwenye vipaji vikali Fally Ipupa. Inama ni ngoma ambayo imetoka mwaka mmoja uliopita na kufanya poa kwenye mtandao wa YouTube kwa kutazamwa na watazamaji milioni 68, kiasi cha kufanya Mondi aonekane bado yuko kileleni.

AFRICAN BEAUTY

Mkwaju mwingine kutoka kwa Mondi wa African Beauty, ambao alivunja rekodi kwa kufanya kolabo na mwanamuziki mkali kutokea nchini Marekani, Omarion.

African Beauty tangu imetoka, ni miaka miwili sasa na tayari imejikusanyia kijiji cha watazamaji milioni 51 mpaka sasa na kuendelea kushikilia rekodi ya ngoma kali ambayo bado haijachuja.

NANA

Mkwaju mwingine mkali wa Nana, Mondi akiwa amemshirikisha staa kutokea nchini Nigeria Mr Flavour, umeachiwa miaka mitano iliyopita na kujikusanyia watazamaji milioni 65 mpaka sasa.

Ni bonge moja la kolabo ambalo Mondi alilitengeneza akiwa na mwanamuziki huyo mkubwa, ambaye naye anafanya vizuri na ngoma zake hata kwenye chati za muziki.

MARRY YOU

Bado Mondi alitikisa tena kwenye ngoma hii kwa kutengeneza kemistri nyingine akiwa na mwanamuziki mkubwa kutokea nchini Marekani Neyo.

Marry You ni ngoma ambayo iliachiwa miaka mitatu iliyopita na kufanya poa kwa kutazamwa zaidi ya mara milioni 44.

Kiwango hicho, kimeifanya ngoma ya Marry You kubaki kwenye chati kali, hasa ukiangalia na mwanamuziki aliyeshirikishwa humo.

SALOME

Salome ni ngoma ya Mondi akiwa na Rayvanny, ambayo nayo ilifanya poa na bado iko kwenye chati. Ngoma hiyo iliachiwa miaka mitatu iliyopita na kutazamwa zaidi ya mara milioni 33 na kuendelea kubaki kwenye ramani nzuri.

SIKOMI

Katika ngoma za Mondi zilizo na rekodi nzuri ya watazamaji, nayo inaingia. Ni ngoma ambayo iliachiwa rasmi miaka miwili iliyopita na ikafanya poa kwa kutazamwa na watazamaji milioni 44 mpaka sasa.

Bado Mondi anaendelea kutikisa na ngoma zake nyingine ambazo zinajizolea watazamaji lukuki kiasi caha kumfanya aendelee kubaki kwenye chati ya wanamuziki wanaofanya poa bara la Afrika na hata kwenye ukanda wa Afrika Mashariki.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *