Kuteuliwa kwa Trump kuwania tuzo amani ya Nobel-unachopaswa kujua

September 11, 2020

Dakika 1 iliyopita

Rais Donald Trump ameteuliwa kwa mara ya pili kuwania tuzo ya amani ya Nobel

Chini ya miezi miwili kabla ya uchaguzi wa Marekani, Rais Donald Trump anaonekana kuwa na jambo la kusheherekea- uteuzi kwa ajili ya tuzo ya amani ya Nobel.

Mwanasiasa wa mrengo wa kulia wa Norway amelipendekeza jina la Trump kuelekea tuzo hizo za mwaka 2021, akieleza kazi ya rais huyo katika mpango wa hivi karibuni wa kuleta amani kati ya Israel na Umoja wa falme za kiarabu.

Christian Tybring-Gjedde alikiambia chombo cha habari cha Fox News siku ya Jumatano : ”Ninafikiri amefanya zaidi katika kutafuta amani kati ya mataifa kuliko ilivyo kwa wateuliwa wengine wa tuzo hii.”

Ameongeza kuwa yeye hakuwa mtu anayemuunga mkono sana Trump,aliongeza. ”Kamati inapaswa kuangalia ukweli na kuamua kwa kutazama ukweli wa mambo, na si kwa namna anavyoonesha tabia zake mara kadhaa.”

Hakika kuteuliwa si sawa na kushinda- hatutamjua mshindi kwa miezi mingine 13 ijayo.

Kwa uteuzi pekee, hakuna kikwazo kikubwa katika kuingia kwenye kinyang’anyiro: Uteuzi kutoka kwa wakuu wa nchi au wanasiasa katika ngazi za kitaifa unakubalika.

Maprofesa wa vyuo vikuu, Wakurugenzi wa Taasisi za sera za mambo ya nje, washiriki waliopita wa tuzo ya Nobel wajumbe wa kamati ya tuzo ya nobel nchini Norway pia ni miongoni mwa wake waliofuzu kuwasilisha uteuzi wao kwa ajili ya tuzo hiyo.Teuzi hizo hazihitaji mualiko

Kwa tuzo ya amani ya Nobel kwa mwaka 2020- mshindi ambaye bado hajatangazwa- kulikuwa na watu 318 wanaowania. Kamati ya Nobel ya Norway haitoi maoni hadharani kuhusu wanaowania, ambao hufanyika kuwa siri.

Je, Trump aliwahi kuteuliwa kabla?

Na kwa mara ya pili, anapaswa kumshukuru Bwaba Tybring-Gjedde. Mwaka 2018, mwanasiasa wa mrengo wa kulia alikua miongoni mwa wabunge wawili waliomchagua Trump kwa ajili ya tuzo hiyo hiyo, kutokana na jitihada za kupatanisha Korea Kaskazini na Korea Kusini.

Trump hakushinda tuzo hiyo mwaka huo, lakini Bwana Tybring-Gjedde, wa chama wa Conservative Progress Party, anasisitiza kuwa Rais Trump awamu hii ametimiza vigezo.

Mwezi uliopita, Israel na UAE walifikia makubaliano ya kusawazisha mahusiano yao, huku Israel ikikubali kuahirisha mipango yake ya kupokonya sehemu ya eneo linalokaliwa la ukingo wa magharibi- hatua iliyotangazwa na Trump.

Rais gani mwingine wa Marekani alishawahi kuteuliwa kwa ajili ya tuzo hiyo?

Trump ni mmoja kati ya marais wa Marekani kupata uteuzi huo, wakiwemo Rais William Howard Taft, Rais Herbert Hoover na Rais Franklin Roosevelt.

Uteuzi wa Obama kwa ajili ya tuzo ya amani ya Nobel ilisababisha ukosoaji mkubwa

Na ikiwa atapata tuzo hiyo, Trump atakuwa rais wa tano wa Marekani kushinda, akiwafuatia Theodore Roosevelt mwaka 1906. Woodrow Wilson mwaka 1920, Jimmy Carter mwaka 2002 na Barack Obama mwaka 2009.

Ushindi wa Obama- ambao uliotokea miezi kadhaa tu akiwa katika wadhifa huo mkubwa – ulikutana na ukosoaji nchini Marekani, huku baadhi wakisema hakuna alichofanya cha kustahili kupata tuzo.

Ruka Twitter ujumbe, 1

Mwisho wa Twitter ujumbe, 1

Miongoni mwao ni bwana Trump ambaye aliandika kwenye ukurasa wake wa Twitter mwaka 2013 akitaka tuzo aliyopatiwa Rais Obama ifutwe.

Katibu Mkuu wa zamani wa kamati ya Nobel Geir Lundestad alisema kuwa anasikitikia uamuzi wa kuchaguliwa kwa Obama. ” Hata wengi wa wanaomuunga mkono Obama wanaona kuwa tuzo hiyo imetolewa kimakosa,” aliliambia shirika la habari la Marekani, AP.

”Kwa hali hii kamati haikufanikiwa kile walichokuwa wakikitarajia.”

Kumekuwa na uteuzi wenye utata hapo awali?

Wakati wapokeaji mashuhuri wa tuzo hiyo ni pamoja na Martin Luther King Jr, Nelson Mandela na Mama Teresa – wote ambao walishinda tuzo – vigezo vya uteuzi vinamaanisha kuwa uteuzi wa zamani ulijumuisha chaguzi zisizo za kawaida, na zenye utata.

Adolf Hitler aliteuliwa kupata tuzo ya amani mnamo 1939 na mbunge wa bunge la Sweden. Iliripotiwa kuwasilishwa kwa kejeli, uteuzi huo uliondolewa muda mfupi baadaye. Miaka michache baadaye, kiongozi wa Kisoviet Josef Stalin aliteuliwa kwa tuzo hiyo hiyo, mara mbili, akijipatia kura za ndio mnamo 1945 – kwa juhudi zake za kumaliza vita vya pili vya dunia -kisha mnamo 1948.

Baada ya kupelekwa kwa teuzi, mpokeaji huchaguliwa na Kamati ya watu watano ya Nobel, ambayo huteuliwa na Bunge la Norway. Mshindi wa tuzo ya 2021 hatatangazwa hadi Oktoba mwakani.

Source link

,Dakika 1 iliyopita Chanzo cha picha, Getty Images Chini ya miezi miwili kabla ya uchaguzi wa Marekani, Rais Donald Trump…

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *