Kura zinaendelea kuhesabiwa Guinea katika uchaguzi wenye utata,

October 19, 2020

Kura zinaendelea kuhesabiwa nchini Guinea katika uchaguzi wa urais, ambapo rais mwenye umri wa miaka 82, Alpha Condé anawania muhula wa tatu wa urais jambo liliozua utata.

Matokeo ya awali yanastahili kutangazwa saa 72 baada ya vituo vya kupiga kura kufungwa, kulingana na sheria ya uchaguzi.

Wagombea watakuwa na siku nane zakuwasilisha malalamishi yao na iwapo watashindwa kufanya hivyo, matokeo ya mwisho wataidhinishwa rasmi bila kupingwa.

Wagombea wanahitaji kupata zaidi ya asilimia 50 ya kura ili kuwa na ushindi wa moja kwa moja vinginevyo kutakuwa marudio ya uchaguzi Novemba 24.

Wagombea wengine kumi wanawania kiti cha urais.

Uchaguzi huo wa Jumapili ulifanyika katika mazingira ya wasiwasi ingawa waziri wa usalama, Damantang Camara amesema hakuna matukio mabaya yaliyorekodiwa.

Pia amewataka wagombea kujizuia kutoa matamshi yasiofaa.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *