Kuna hofu kwamba nchi ya Ethiopia huenda ikagawanyika

September 7, 2020

Dakika 3 zilizopita

Vikosi maalumu vya kijeshi vikiwa vimekusanyika wakati kukiwa na makabiliano

Mgogoro kati ya Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed na chama tawala kuhusu eneo la kimkakati la Tigray huenda unaendelea kuongezeka na kuzua wasiwasi wa kutokea kwa makabiliano ya jeshi na kugawanyika kwa taifa hilo ambalo ni la pili kwa wingi wa watu Afrika.

Wasiwasi huo unazunguka uamuzi wa serikali za maeneo wa kuendelea na maandilizi ya uchaguzi wao wa bunge la Tigray Jumatano, ikiwa ni hatua ambayo haijawahi kufanyika hapo kabla inayokwenda kinyume na serikali kuu.

Hii ni ishara ya hivi karibuni kwamba Bwana Abiy ana wakati mgumu wa kuendeleza sifa yake kama mpatanishi wa amani – takribani mwaka mmoja baada ya kushinda tuzo la Amani la Nobel kwa kumaliza vita vya mpakani na Eritrea na juhudi zake kwa kufanya Ethiopia kuwa ya demokrasia.

Watu karibu 9,000 wamekamatwa nchini Ehtiopia katika mapigano makali baada ya mauaji ya muimbaji Hachalu Hundessa mwezi Juni, wanaharakati wa haki za binadamu wanasema, na kupelekea wasiwasi wa kwamba huenda utawala wa dikteta ukarejea tena wakati ambapo Waziri Mkuu aliahidi kuumaliza alipoingia madarakani 2018.

Sababu ya wasiwasi ni nini?

Chama tawala katika eneo hilo, Tigray People’s Liberation Front (TPLF), kilisababisha msukosuko wa kisiasa kilipotangaza kwamba kitafanya uchaguzi wa wabunge wa eneo utafanyika licha ya serikali kuu na tume ya uchaguzi kutangaza kuwa uchaguzi huo umeahirishwa.

Tangu kumalizika kwa utawala wa Maksi mwaka 1991 na hadi hivi karibuni, chama cha TPLF kimekuwa kwenye muungano unaoegemea ukabila ambapo kila chama hudhibiti eneo lake katika serikali kuu. Kwahiyo kutofikiwa kwa makubaliano na Bwana Abiy ni mpasuko mkubwa katika ngazi ya uongozi nchini humo.

Mkazi wa mji wa Mekelle akiwa juu ya farasi aliyepakwa rangi za bendera ya eneo la Tigray

Chama cha TPFL kimesema kwamba makundi ya upinzani yanayoongozwa na Abiy yanastahili kuvunjwa mwezi huu kwasababu wakati ambapo muhula wa bunge anafikia ukomo wake na kuahirishwa kwa uchaguzi ambao ulikuwa unastahili kuwa umefanywa kufikia Agosti, ni ukiukaji wa katiba na kuanza kuzua wasiwasi kwamba huenda huo ukawa mwanzo wa kutamatika kwa utawala wa Bwana Abiy.

Washirika wa Bwana Abiy, walisema kwamba tume ya uchaguzi imeahirisha uchaguzi kwasababu ya mlipuko wa virusi vya corona, na sio kwasababu waziri mkuu anataka kuingia madarakani, kama vyama upinzani vinavyodai.

Upinzani unasema kwamba bado anasalia kuwa mtawala halali kwasababu muda wa uongozi wa bwana Abiy uliongezwa kwa miezi 12, tangu janga la corona lilipojitokeza kuwa tishio.

Umuhimu wa uchaguzi wa TPLF ni upi?

Kumezuka wasiwasi kwamba chama cha TPLF huenda kinatengeneza mazingira ya kuwepo kwa mpasuko, huku bunge na serikali zikiingia madarakani bila baraka za serikali kuu.

Chama cha TPLF kinasisitiza kwamba kimejitolea kuendeleza uhusiano wake na Ethiopia lakini kitalinda utawala wale na kupinga kile inachokiita jaribio la Abiy la kujenga taifa linalotegemea maamuzi ya upande mmoja.

“Hatuwezi kurejea nyumba kwa yeyote ambaye anadhamiria kukandamiza haki yetu tulioipigania kwa bidii zote kwa malengo na utawala wa mtu binafsi,” kiongozi wa eneo, Debretsion Gebremichael, alisemahivyo mwezi uliopita.

Wanajeshi wa vikosi maalum walitawanywa kwenye miji mikubwa ikiwemo Mekelle

Taarifa yake iliwadia siku chache baada ya vikosi vya usalama – vilivyokuwa vimejihami kwa bunduki za rashasha na kurusha roketi – kuandamani katika miji mikuu ya Tigray ishara wasiwasi kwamba huenda kukawa na makabiliano ya kijeshi.

“Tuko tayari kulipa kwa ajili ya amani,” ofisi ya usalama wa eneo iliandika kwenye mtandao wa Facebook siku ya maandamano

Jibu la serikali ya Bwana Abiy ni lipi?

Serikali imetangaza kwamba uchaguzi wa Tigray ni kinyume cha sheria na kuongeza kwamba tume ya uchaguzi ndio pekee yenye nguvu ya kuandaa uchaguzi.

Maandalizi ya uchaguzi

Hata hivyo, Bwana Abiy ameondoa uwezekano wa kutuma vikosi vya jeshi eneo hilo kuzuia uxhaguzi na kusema kwamba uamuzi wa aina hiyo utakuwa uenda wazimu.

“Serikali kuu haina nia na shauku yoyote ya kushambulia watu wake,” alisema Julai 25.

Lakini wenye msimamo mkali wanaompendelea Abiy, ikiwemo aliyekuwa mkuu wa jeshi Kassaye Chemeda, ametoa wito wa muingilio wa jeshi huko Tigray.

“Serikali inastahili kupanga vizuri na wanastahili kushambuliwa,” alisema katika mahojiano na televisheni yenye kuhusishwa na serikali ya Walta TV.

Ikijibu wito kutoka kwa bunge la juu la serikali kukutana Jumamosi kuzungumzia uchaguzi wa Tigray, serikali ya eneo ilionya kwamba uamuzi wowote wa kuzuia au kutatiza uchaguzi wa eneo ni sawa na kutangaza vita”.

Aidha, Wabunge wa Tigraya wa bunge la juu wamesema kwamba watasusia mkutano huo.

Kwanini uchaguzi umezorota kiasi hicho?

Chama cha TPLF – ambacho kilikuwa na ushawishi mkubwa katika serikali kuu tangu utawala wa Maksi kumalizika 1991, huku kiongozi wake, Meles Zenawi, aliyehudumu kama waziri mkuu kutoka 1995 hadi 2012 – kimehisi ukosefu wa madaraka chini ya utawala wa Bwana Abiy hasa baada ya maafisa wa jeshi na usalama ama waliondolewa au kukamatwa muda mfupi baada ya Bwana Abiy kuingia madarakani 2018 kufuatia maandamanp makubwa dhidi ya utawala uliotangulia.

Picha iliyopigwa Julai 6, 2019 inaonesha mji wa Mekelle Ethiopia

Maelezo ya picha,

Former Prime Minister Meles Zenawi had strong support in Mekelle, the capital of Tigray.

Aliyekuwa mkuu wa idara ya upelelezi Getachew Assefa alifanikiwa kuepuka kukamatwa na kusemekana kwamba amekimbia Tigray.

Ushawishi wa chama cha TPLF ulizorota zaidi hasa baada ya Bwana Abiy kuzindua chama chake cha Prosperity – muungano wa vyama vya kikabila uliotumika kuunda chama tawala.

Chama cha TPLF kilikataa kujiunga na PP na kukiacha bila ushawishi wowote katika serikali kuu kwa mara ya kwanza tangu kumalizika kwa utawala wa Maksi. Bwana Abiy aliwafuta kazi baadhi ya wanachama wa chama hicho katika baraza la mawaziri huku wengine wakijiuzulu.

Matokeo yake, chama cha TPLF pia kimeachana na makao yake makuu ya eneo, Mekelle, na kuzua wasiwasi kwamba ushirikiano na sehemu nyingine za Ethiopia ulikuwa unatetereka.

Serikali kuu ilianza kamata kamata ya raia baada ya mauaji ya mwanamuziki Hachalu na kusababisha baadhi ya wakosoaji wake kusema kwamba hatua hiyo imesababisha mwamo wa kisaikolojia ndani ya chama cha TPLF.

Vikosi vya usalama vilivamia na kufunga ofisi za televisheni iliyokuwa inahusishwa na chama cha TPLF, Dimtsi Woyane, katika mji mkuu. Pia ilifunga kituo cha televisheni cha Oromo Media Network, ambacho kinahusishwa na mwanasiasa wa upinzani aliyekizuizini Jawar Mohammed.

Maafisa wa serikali na chama cha Prosperity kinachoongozwa na Bwana Abiy, wanashutumu chama cha TPLF kwa mauaji ya mwanamuziki Hachalu na kufanya kila mbinu kugawanya nchi.

Chama cha TPLF kilijibu kwa kusema kwamba chama hicho kinatumiwa kama chambo kwa ukosefu wa uongozi thabiti wa Bwana Abiy na yote mabaya yaliosababishwa na utawala wake.

Je tishio la kutaka kujitenga likoje?

Chama cha TPFL kilikuwa na jukumu muhimu katika kung’atua mamlakani utawala wa Maksi mwaka 1991, na pia kwenye uundwaji wa katiba ambako kulitoa haki ya maeneo kujitegemea.

Ingawa chama hicho hakijawahi kuonesha nia ya eneo la Tigray kutaka kujitenga, kila wakati kimekuwa kikisema kwamba haki yake inastahili kuheshimiwa.

Wafuasi wa chama cha TPLF

Aidha, kuna chama kipya cha upinzani ambacho kimeibuka, cha Tigray Independence Party (TIP), katika uchaguzi wa eneo na kimesema kwamba nia yake ni kukomboa uhuru wa Tigray.

Chama hicho kilikuwa katika vita vya mapigano ya mpaka wa Ethiopia na Eritrea mwaka 1998.

Makumi ya maelfu ya watu waliuawa katika mapigano hayo baada ya Eritrea kuanzisha mashambulizi ya kutwaa tena udhibiti wa mji wa Badme eneo la Tigray.

Bwana Abiy alsaini makubaliano ya Amani na rais wa Eritrea Isaias Afwerki kumaliza vita kati ya nchi hizo mbili”, na hatimae mpaka kati ya nchi hizo mbili ukafunguliwa.

Ramani
Maelezo ya picha,

The Ethiopia-Eritrea border dividing families

Hata hivyo, kufuka mipaka kumefungwa tena.

Idhaa hali katika mji wa Badme bado haijapata ufumbuzi. Eritrea inataka Ethiopia kutekeleza sheria za Umoja wa Mataifa ili iweze kukabidhi mji huo.

Lakini hili haliwezi kufikiwa bila ya ushirikiano wa serikali eneo la Tigray, kwasababu ni utawala wa eneo.

Kwahiyo, rais wa Ethiopia Abiy Ahmed mshindi wa tuzo ya Amani ya Nobel, huenda akawa na wakati mgumu kufikia Amani ya kudumu na Eritrea, kwasababu kwanza atahitajika kutatua tofauti yake na TPLF.

Source link

,Dakika 3 zilizopita Mgogoro kati ya Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed na chama tawala kuhusu eneo la kimkakati la…

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *