Korti ya Katiba Ivory Coast yamruhusu Rais Ouattara kugombea muhula wa tatu, on September 15, 2020 at 8:00 am

September 15, 2020

Mahakama ya katiba ya Ivory Coast imemsafishia njia rais wa nchi hiyo Alassane Ouattara kugombea muhula wa tatu. Uamuzi huo umefuatiwa na maandamano yenye ghasia, yanayotishia kuitumbukiza nchi hiyo ya Afrika magharibi katika machafuko mithili ya yale ya muongo mmoja uliopita, ambayo yaliangamiza maisha ya watu zaidi ya 3000. Aidha, mahakama hiyo hiyo imemzuia rais wa zamani Laurent Gbagbo, na kiongozi wa zamani wa waasi Guillaume Soro kugombea urais katika uchaguzi ujao. Majaji wa mahakama hiyo wameridhia wagombea wanne tu kati ya 44 waliotia nia ya kuwania urais katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 31. Miongoni mwa walioruhusiwa kusimama dhidi ya Ouattara no Konan Bedie, rais wa zamani wa Ivory Coast ambaye sasa anao umri wa miaka 86. Waandamanaji wenye hasira walichoma magari katika miji ya Yopougon na Bangolo, kufuatia makabiliano baina ya wafuasi wa upinzani na maafisa wa usalama.,

Mahakama ya katiba ya Ivory Coast imemsafishia njia rais wa nchi hiyo Alassane Ouattara kugombea muhula wa tatu. 

Uamuzi huo umefuatiwa na maandamano yenye ghasia, yanayotishia kuitumbukiza nchi hiyo ya Afrika magharibi katika machafuko mithili ya yale ya muongo mmoja uliopita, ambayo yaliangamiza maisha ya watu zaidi ya 3000. 

Aidha, mahakama hiyo hiyo imemzuia rais wa zamani Laurent Gbagbo, na kiongozi wa zamani wa waasi Guillaume Soro kugombea urais katika uchaguzi ujao. 

Majaji wa mahakama hiyo wameridhia wagombea wanne tu kati ya 44 waliotia nia ya kuwania urais katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 31. 

Miongoni mwa walioruhusiwa kusimama dhidi ya Ouattara no Konan Bedie, rais wa zamani wa Ivory Coast ambaye sasa anao umri wa miaka 86. 

Waandamanaji wenye hasira walichoma magari katika miji ya Yopougon na Bangolo, kufuatia makabiliano baina ya wafuasi wa upinzani na maafisa wa usalama.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *