Korea kusini yaonesha hofu ya silaha za Korea kaskazini

October 11, 2020

Silaha za Korea kaskazini zilizooneshwa ni makombora mapya ya masafa marefu  katika  gwaride la kijeshi  

Wakati wa sherehe  za  kuadhimisha miaka 75  tangu kuasisiwa chama  tawala  mjini  Pyongyang jana Jumamosi, Korea  kaskazini ilionesha  aina  mbali  mbali  za  mifumo  ya  silaha, ikiwa  ni  pamoja na  makombora  mawili  ambayo  yameoneshwa  hadharani  kwa mara  ya  kwanza  kwa  mataifa  ya  nje.

Nordkorea Kim Jong Un inspiziert den Bau eines U-Boots (KCNA/AP Photo/picture-alliance)

Kiongozi wa Korea kaskazini Kim Jong Un aizungumza na waandishi habari

Moja  ni  lile  ambalo  lilionekana  kama  kombora la  masafa marefu linaloweza  kufika  katika  bara  jingine ambalo  ni  kubwa  kuliko kombora  lolote  la  Korea  kaskazini  linalofahamika  la  masafa marefu linalofika  katika  bara jingine, ICBM, na  lingine  linaonekana kama  ni  aina iliyofanyiwa mabadiliko  ambalo  linaweza  kufyatuliwa kutoka  katika  nyambizi.

Wakati baadhi ya  wataalamu  wanasema   inaweza kuwa ni makombora ya mfano tu ambayo yanaendelea  kufanyiwa kazi, kuoneshwa kwao  hadharani  kunaonesha kuwa Korea kaskazini imekuwa  ikiendelea  kusogea  mbele  katika  kuimarisha  uwezo wake  wa  silaha huku  kukiwa  na  mkwamo katika  diplomasia  ya nyuklia na  Marekani.

Wizara ya  ulinzi  ya  Korea  kusini imesema  leo inaeleza wasi wasi wake juu  ya  ukweli  kwamba “Korea kaskazini  imeonesha  silaha ikiwa  ni  pamoja  na  zile zilizokuwa zinashukiwa  kuwa  makombora mapya  ya  masafa marefu.” Taarifa  ya  wizara  iliitaka  Korea kaskazini  kuendelea  kuwa  sehemu  ya  makubaliano  ya  pamoja ya  Korea  ya  mwaka  2018 yenye lengo  la  kupunguza  uadui baina yao.

Vietnam Hanoi | Treffen Kim Jong-Un und Donald Trump (picture-alliance/AP Photo/E. Vucci)

Kiongozi wa Korea kaskazini Kim Jogn Un (kushoto) na Donald Trump (kulia)

Mazungumzo ya kinyuklia

Wizara ya  mambo  ya  kigeni  ya  Korea  kusini imetoa  taarifa tofauti  inayoitaka  Korea  kaskazini  kurejea  katika  mazungumzo  ili kupata kupiga  hatua  katika  nia yake  thabiti ya  kufikia kutokuwa na silaha za  kinyuklia na  amani  katika  rasi ya  Korea.

Baada  ya mkutano wa  dharura wa  baraza  la  usalama  la  taifa, wajumbe wa baraza hilo  nchini Korea  kusini  walisema wataendelea  na  kufanya  tathmini ya  umuhimu wa  mkakati  wa mfumo  wa  silaha wa Korea  kaskazini  uliooneshwa  jana na kufanya  mapitio mapya  ya  uwezo wa  ulinzi  wa  Korea  kusini.

Mahusiano kati ya  Korea  mbili yanaendelea  kuwa  mabaya  huku kukiwa  na  mkwamo  wa  diplomasia  ya  kinyuklia kati ya Pyongyang na  Washington.

Nordkorea Raketentest (picture-alliance/AP Photo/Korean Central News Agency)

Jaribio la kombora Korea kaskazini

Katika  hotuba  iliyotolewa  wakati wa  gwaride  hilo  la  kijeshi, kiongozi  wa  Korea  kaskazini  Kim Jong Un alionya  kwamba atatumia uwezo wake wote wa  kinyuklia iwapo atatishiwa  lakini aliepuka  kuikosoa  moja  Marekani.

Ukweli  kwamba Kim anaendelea na hatua alizoziweka  binafsi  za kuzuwia majaribio ya  makombora  ya  masafa  marefu ya  kinyuklia bado  anataka  kuweka  nafasi za  kidiplomasia hai  na  Marekani . Lakini  baadhi ya  wataalamu  wanasema  atafanya  jaribio  kubwa la  silaha  baada  ya  uchaguzi  wa  rais  wa  Marekani  hapo Novemba kuimarisha  nafasi yake  katika  majadiliano  mapya  na Marekani , kwa  yeyote  atakayeshinda  uchaguzi.

 

Source link

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *