Konyagi yabadilishwa mwonekano, ladha ile ile

October 18, 2020

 

Kampuni ya Bia nchini TBL kupitia kinywaji chake cha konyagi imezindua nembo mpya ya kinywaji hicho inayoipa muonekano mpya ili kuendelea kuvutia wateja wake kutokana na kinywaji hicho kuwa na msisimko wa kipekee na wa hali ya juu.

Akizungumza na waandishi wa habari katika uzinduzi wa nembo hiyo uliofanyika jana usiku Jijini Dar es Salaam Meneja wa bidhaa hiyo Pamela Kikuki amesema, uzinduzi wa nembo hiyo unaenda sambamba na kauli mbiu ya kinywaji hicho iliyopewa jina la ‘Konyagi Washa Cheche’

“Kinywaji hiki cha konyagi hakijabadilika bali kimeongezewa vionjo vya kimuonekano na ladha ni ile ile na kuwaomba watumiaji kutumia kinywaji hicho bila wasiwasi wowote”, amesema Bi.Pamela

Kwa upande mwingine Pamela amesema konyagi ni kinywaji aina ya Gin ilioanza kutengenezwa mwaka 1977 na ladha yake ikiwa ni ile ile ila wao wamebadilisha muonekno pekee.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *