Kombe asili la Matifa ya Afrika limepotea nchini Misri

September 6, 2020

Ahmed Hassan of Egypt

Maelezo ya picha,

Nahodha wa Misri Ahmed Hassan akishikilia Kombe la mataifa baada ya kushinda fainali mwaka 2010

Uchunguzi umeanzisha na Shirikisho la soka la Misri FA (EFA) baada ya kubaini kuwa vikombe kadhaa vimepotea kutoka makao makuu yake mjini Cairo, likiwemo kombe asili la Mataifa ya Afrika.

Misri ilipokea zawadi ya kombe hilo iposhinda michuano ya 2010, kwa kuwa ilikuwa imeshinda kombe la aina hiyo kwa mara ya tatu.

Kombe hilo ambalo mtindo wake ulitumiwa kwa mara ya kwanza mwaka 2002 baada ya Cameroon kupewa kombe la awali baada ya kushinda mara tatu shindano hilo, lilitolewa kwa EFA na shirikisho la soka la Afrika (Caf) baada ya kupata ushindi mara tatu mwaka 2006, 2008 na 2010.

Ijumaa Shirikisho la soka la Misri EFA – ambalo mkurugenzi wake wa habari aliithibitishia BBC kupotea kwa kombe hilo – alisema wameanzisha uchunguzi juu ya kupotea kwa vikombe mbalimbali.

“Wakati Chama cha Soka cha Misri kwa sasa kinafanya ujenzi makao yake makuu , ikiwa ni pamoja na kubadilisha lsehemu ya lango kuu la kuingia kwenye makumbusho madogo ya soka ya Misri, utawala wake umeshitushwa na kupotea kwa baadhi ya vikombe katika chumba maalumu cha kuhifadhia vikombe ,” taarifa ya EFA imesema.

Baada ya kushambuliwa kwa makao makuu ya EFA mwaka 2013, vikombe mbali mbali -likiwemo Kombe la Mataifa ya Afrika -vilihamishiwa kwenye chumba kingine maalum.

Mwaka 2010 Misri ilipewa dhamana ya kuweka kombe hilo daima baada ya kushinda mara tatu mfulurizo

Maelezo ya picha,

Mwaka 2010 Misri ilipewa dhamana ya kuweka kombe hilo daima baada ya kushinda mara tatu mfulurizo

Hatahivyo, maafisa nchini humo walivitafuta vikombe hivyo hivi karibuni tu, baada ya uamuzi wa kukarabati lango la EFA ili vikombe vingi ambavyo Misri imevipata viwekwe eneo la kuingia kwa ajili ya maonyesho.

Uvamizi wa EFA na mashabiki wenye jazba miaka saba iliyopita wakati wa ghasia mjini Cairo kwa sasa ni suala linaoangaliwa huku maafisa wakijaribu kubaini ni lini na ni vipi vikombe hivyo vilichukulia.

” Kwa sasa EFA inachunguza ‘ kutoweka kwa vikombe ili kubaini kama vilikombe hivyo vya zamani vilichukuliwa wakati jengo lilipoungua…au kama vilipoteawakati jengo lilipovamiwa wakati wa tukio ,” EFA iliongeza.

Kulingana na sheria za Caf nchi ambayo timu yake inashinda kombe fulani la Mataifa ya Afrika mara tatu, timu hiyo inalimiliki moja kwa moja.

The former style of the Africa Cup of Nations trophy

Maelezo ya picha,

Muundo wa kombe la zamani la Matifa ya Afrika ambalo lilitolewa kwa Cameroon mwaka 2000

Ghanailikuwa ni nchi ya kwanza kushinda mara tattu, mwaka 1978, halafu Cameroon ambayo ilipokea kikombe cheny muundo mwingine wa kombe la Mataifa ya Afrika baada ya kuwa nchi ya kwanza kushinda kombe hilo kwa mara tatu.

Chini ya sheria za Caf, timu inayoshinda hupokea Kombe la Mataifa ya Afrika linalofanana na kombe asili na kulimiki daima huku wakiruhusiwa kulitunza kwa miaka miwili kabla ya kulikabidhi tena.

Kombe la sasa ambalo mtindo wake bado ni sawa na lile ambalo Misri ililitwaa, liko mikononi mwa Algeria, ambao walishinda taji la Kombe la Mataif ya Afrika (mjini Cairo) mwaka jana.

Source link

,Dakika 1 iliyopita Chanzo cha picha, Getty Images Maelezo ya picha, Nahodha wa Misri Ahmed Hassan akishikilia Kombe la mataifa…

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *