Kocha yanga awavaa wachesaji kisa hiki hapa, on September 17, 2020 at 6:00 am

September 17, 2020

 KOCHA Mkuu wa Yanga, Zlatko Krmpotic amewajia juu wachezaji wake kwa kusema kuwa haridhishwi na kiwango cha mabao ambayo timu yake inafunga.Yanga mpaka sasa kwenye michezo miwili ya Ligi Kuu Tanzania Bara imefanikiwa kufunga mabao mawili na kujiwekea kibindoni pointi nne kati ya sita ambazo zlikuwa zinasakwa uwanjani.Ilifanikiwa kutoka sare ya bao 1-1 na Prisons na mchezo wa wikiendi iliyopita ilipata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Mbeya City, kitu ambacho hakimfurahishi kocha huyo. Krmpotic amesema haitoshi tu kwa timu kumiliki mpira muda mwingi bali ni lazima wachezaji wake wabadilike na kutengeneza nafasi za kufunga mabao zaidi.“Katika michezo miwili ambayo timu yangu imecheza mpaka sasa kwenye ligi tumefunga mabao mawili pekee, kama kocha siridhishwi na hali hiyo kwa kuwa inaonyesha dhahiri wachezaji wangu hasa wanaocheza kwenye robo ya mwisho ya uwanja wanakosa ubunifu wa kutengeneza nafasi.“Mfano mzuri ni namna ambavyo tulicheza mchezo wetu uliopita dhidi ya Mbeya City ambapo tulishambulia kwa dakika 75, lakini hatukuweza kutengeneza nafasi za wazi ambazo tungezigeuza kuwa mabao jambo ambalo ni lazima tulifanyie kazi haraka kabla hatujatoka kuanza michezo yetu ya ugenini,” amesema Krmpotic.Wachezaji wanaolalamikiwa na kocha huyo ni Michael Sarpong, Sogne Yocouba, Ditram Nchimbi, Deus Kaseke, Tuisila Kisinda, Haruna Niyonzima, Carlos Carlinhos na Farid Musa.Yanga Jumamosi hii ya Septemba 19 inatarajia kuwa mgeni wa Kagera Sugar mchezo utakaopigwa kwenye Uwanja wa Kaitaba Mkoani Kagera.,

 

KOCHA Mkuu wa Yanga, Zlatko Krmpotic amewajia juu wachezaji wake kwa kusema kuwa haridhishwi na kiwango cha mabao ambayo timu yake inafunga.

Yanga mpaka sasa kwenye michezo miwili ya Ligi Kuu Tanzania Bara imefanikiwa kufunga mabao mawili na kujiwekea kibindoni pointi nne kati ya sita ambazo zlikuwa zinasakwa uwanjani.

Ilifanikiwa kutoka sare ya bao 1-1 na Prisons na mchezo wa wikiendi iliyopita ilipata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Mbeya City, kitu ambacho hakimfurahishi kocha huyo.

 Krmpotic amesema haitoshi tu kwa timu kumiliki mpira muda mwingi bali ni lazima wachezaji wake wabadilike na kutengeneza nafasi za kufunga mabao zaidi.

“Katika michezo miwili ambayo timu yangu imecheza mpaka sasa kwenye ligi tumefunga mabao mawili pekee, kama kocha siridhishwi na hali hiyo kwa kuwa inaonyesha dhahiri wachezaji wangu hasa wanaocheza kwenye robo ya mwisho ya uwanja wanakosa ubunifu wa kutengeneza nafasi.

“Mfano mzuri ni namna ambavyo tulicheza mchezo wetu uliopita dhidi ya Mbeya City ambapo tulishambulia kwa dakika 75, lakini hatukuweza kutengeneza nafasi za wazi ambazo tungezigeuza kuwa mabao jambo ambalo ni lazima tulifanyie kazi haraka kabla hatujatoka kuanza michezo yetu ya ugenini,” amesema Krmpotic.

Wachezaji wanaolalamikiwa na kocha huyo ni Michael Sarpong, Sogne Yocouba, Ditram Nchimbi, Deus Kaseke, Tuisila Kisinda, Haruna Niyonzima, Carlos Carlinhos na Farid Musa.

Yanga Jumamosi hii ya Septemba 19 inatarajia kuwa mgeni wa Kagera Sugar mchezo utakaopigwa kwenye Uwanja wa Kaitaba Mkoani Kagera.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *