Kocha wa Yanga atoa angalizo, noreply@blogger.com (Muungwana Blog 3), on September 1, 2020 at 10:00 am

September 1, 2020

Kocha msaidizi wa Klabu ya Yanga, Juma Mwambusi amesema wanahitaji muda kukijenga kikosi cha ushindani katika msimu wa mashindano unaotarajiwa kuanza septemba tisa mwaka huu.Mwambusi ambaye aliwahi kuifundisha miamba hiyo ya soka nchini akiwa na Makocha Hans Van Pluijm na George Lwandamina kwa nyakati tofauti,alirejeshwa hivi karibuni na sasa ndiye msaidizi wa mserbia Zlatko Krmpotik ambaye aliwasili siku ya Ijumaa.”Kusema ukweli tuna wachezaji wazuri,lakini kwa idadi yao kubwa inabidi tupate muda wa kutosha ili kuwaunganisha,ingawa kwa bahati mbaya ligi inaanza keshokutwa,ni ngumu sana,na hata kocha mkuu alisemaatahitaji muda ila bahati mbaya Yanga haitohitaji hilo zaidi ya matokeo””Sidhani kama tutapata muda wa kucheza mechi za kirafiki,ligi inaanza tarehe sita,inawezekana mchezo dhidi ya Eagle Noir ilifaa kufanya angalau tathmini ya wachezaji,hivyo tusubiri tuone itakuaje”Yanga itafungua dimba kwa kumenyana na Tanzania Prisons mchezo utakaopigwa tarehe saba ya mwezi huu siku ya jumapili katika uwanja wa Mkapa Jijini Dar es salaam.,

Kocha msaidizi wa Klabu ya Yanga, Juma Mwambusi amesema wanahitaji muda kukijenga kikosi cha ushindani katika msimu wa mashindano unaotarajiwa kuanza septemba tisa mwaka huu.

Mwambusi ambaye aliwahi kuifundisha miamba hiyo ya soka nchini akiwa na Makocha Hans Van Pluijm na George Lwandamina kwa nyakati tofauti,alirejeshwa hivi karibuni na sasa ndiye msaidizi wa mserbia Zlatko Krmpotik ambaye aliwasili siku ya Ijumaa.

”Kusema ukweli tuna wachezaji wazuri,lakini kwa idadi yao kubwa inabidi tupate muda wa kutosha ili kuwaunganisha,ingawa kwa bahati mbaya ligi inaanza keshokutwa,ni ngumu sana,na hata kocha mkuu alisemaatahitaji muda ila bahati mbaya Yanga haitohitaji hilo zaidi ya matokeo”

”Sidhani kama tutapata muda wa kucheza mechi za kirafiki,ligi inaanza tarehe sita,inawezekana mchezo dhidi ya Eagle Noir ilifaa kufanya angalau tathmini ya wachezaji,hivyo tusubiri tuone itakuaje”

Yanga itafungua dimba kwa kumenyana na Tanzania Prisons mchezo utakaopigwa tarehe saba ya mwezi huu siku ya jumapili katika uwanja wa Mkapa Jijini Dar es salaam.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *