Kocha wa Bremen azungumzia hali tete ya kifedha klabuni

October 8, 2020

Klaassen  amerejea  katika  klabu ya  Ajax Amsterdam  katika  siku ya  mwisho  ya  uhamisho siku ya Jumatatu kwa kitita cha  euro milioni 11. Pia  wanalenga  kumuuza  Milot Rashica  kwa  Bayer Leverkusen hali  ambayo  hata  hivyo  haikuweza  kufanikiwa.

 

“Hatujafikia  lengo  letu la  uhamisho kwa mtazamo wetu  wa  kispoti, ” Kohfeldt amesema baada  ya mchezo wa  kirafiki dhidi  ya  St Pauli Hamburg, usiku wa  Jumatano.

Fußball Bundesliga Werder Bremen - Arminia Bielefeld (Carmen Jaspersen/dpa/picture-alliance)

Wachezaji wa Werder Bremen

“Lakini Werder Bremen imo  katika   hali  mbaya  ya  kifedha. Kila mmoja  ni  lazima  atambue hilo, na  kila  mmoja  ni  lazima apambane.”

Maingwa hao wa zamani wa Bundesliga  wameathirika  pakubwa  na janga  la  virusi vya  corona na  uwanjani waliepuka  tu  kushuka daraja  msimu uliopita  katika  mpambano wa  mchujo dhidi ya timu ya  daraja  la  pili.
 

Wameanza msimu  mpya kwa  ushindi  mara  mbili kutoka michezo mitatu lakini Kohfeldt  alisema wanapaswa kuimarika “kutokana  na hali ya juu ya kitisho” katika  michezo.

 

Source link

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *