KMC kuivaa Mwadui kesho uwanja wa Mwadui Complex, on September 20, 2020 at 1:11 pm

September 20, 2020

 Kikosi cha Timu ya  ya Manispaa ya Kinondoni, KMC FC kimejiandaa vilivyo katika  kukabiliana na mchezo wake wa kesho dhidi ya Mwadui FC ya Mkoani Shinyanga mchezo utakaopigwa katika Dimba la Mwadui Complex Mkoani humo.Kikosi hicho ambacho kimeweka kambi Mkoani humo leo kimefanya mazoezi katika uwanja wa Kambarage Mkoani Shinyanga ikiwa ni katika hatua za mwisho kabla ya kuelekea kwa mchezo huo ambao KMC FC itakuwa mgeni  dhidi ya Mwadui FC.Katika kikosi hicho hali ya wachezaji ni nzuri na kwamba hakuna majeruhi ambaye anaweza kukosa mchezo huo ambao KMC imejipanga kuhakikisha kwamba inapata ushindi wa alama tatu kwa lengo la kuendelea kuongoza ligi kuu inayoendelea hapa Nchini.,

 Kikosi cha Timu ya  ya Manispaa ya Kinondoni, KMC FC kimejiandaa vilivyo katika  kukabiliana na mchezo wake wa kesho dhidi ya Mwadui FC ya Mkoani Shinyanga mchezo utakaopigwa katika Dimba la Mwadui Complex Mkoani humo.

Kikosi hicho ambacho kimeweka kambi Mkoani humo leo kimefanya mazoezi katika uwanja wa Kambarage Mkoani Shinyanga ikiwa ni katika hatua za mwisho kabla ya kuelekea kwa mchezo huo ambao KMC FC itakuwa mgeni  dhidi ya Mwadui FC.

Katika kikosi hicho hali ya wachezaji ni nzuri na kwamba hakuna majeruhi ambaye anaweza kukosa mchezo huo ambao KMC imejipanga kuhakikisha kwamba inapata ushindi wa alama tatu kwa lengo la kuendelea kuongoza ligi kuu inayoendelea hapa Nchini.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *