Kizito Mihigo: Mwimbaji wa Rwanda atuzwa ‘kwa kupinga udikteta’

September 18, 2020

Dakika 1 iliyopita

Kizito Mihigo

Maelezo ya picha,

Kizito Mihigo alihoji maelezo rasmi kuhusu mauaji ya kimbari ya Rwanda

Kizito Mihigo ndiye mshindi wa tuzo ya kimataifa ya Havel mwake 2020, ambayo inawaenzi “wanaharakati wanaotumia ubunifu wao katika sanaa kupinga uongozi wa kiimla”, Wakfu wa Haki za Binadamu(HRF) unasema.

Bwana Kizito ambaye alifariki ndani ya seli ya polisi mjini Kigali mwezi Februari, ni mtu wa kwanza kupewa tuzo hiyo akiwa hayupo duniani tangu ilipozinduliwa mwaka2012.

Wakfu wa HRF unasema Kizito – manusura wa mauaji ya kimbari nchini Rwanda- “alionesha ujasiri katika wimbo wake wa mwaka 2014 ” ambao aliutunga kuwafariji “wale waliouawa na vikosi vya RPF baada ya mauaji ya kimbari ya waka 1994”.

“Mihigo alitoa wimbo huo akiwa na ufahamu kwamba utamletwa matatizo,” taarifa ya Human Rights Foundation ilisema.

Ushindi huo umepokelewaje?

Tumepokea taarifa hizi kwa mshangao na furaha sisi hapa katika ofisi za KM”, Delphine Uwituze kiongozi wa wakfu wa Kizito Mihigo (KMP) alisema.

“Tumefurahi sana kwamba ulimwengu sasa unatambua juhudi za Kizito kuleta Amani na maridhiano nchini Rwanda” -Bi Uwituze aliiambia BBC.

Mshindi wa tuzo ya kimataifa ya Havel hupokea sanamu ya shaba ambayo inaashiria “mungu wa kike wa Demokrasia,” na zawadi ya pesa taslimu ya dola 38,000, kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na HRF.

Wengine waliotambuliwa katika toleo la mwaka 2020 ya tuzo hiyo ni Omar Abdulaziz, mchekeshaji anayeangazia siasa za Saudi Arabia mwenye makao yake nchini Canada pamoja na msanii Badiucao raia wa China aliyepo ufichoni Australia, ilisema taarifa ya HRF iliongezea kusema.

Mwanamuziki maarufu kwa nyimbo za injili nchini Rwanda Kizito Mihigo

Maelezo ya picha,

Mwanamuziki maarufu kwa nyimbo za injili nchini Rwanda Kizito Mihigo

Kifo cha ghafla cha bwana Kizito Mihigo kilizua gumzo ndani na nje ya Rwanda.

Mamlaka nchini Rwanda zilisema kuwa msani huyo alijiua alipokuwa anazuiliwa mahabusu katika kituo cha polisi.

Kizito Mihigo alikuwa anazuiliwa kwa madai ya kujaribu kuvuka mpaka kiharamu kungia Burundi.

Hatahivyo wanaharakati wanaoishi ughaibuni wamepinga taarifa iliotolewa na polisi hao.

Wamesema kwamba mwanamuziki huyo hakutaka kujiunga na kundi la waasi nchini Burundi na kwamba alitaka kwenda Ubelgiji ambapo alikuwa akiishi .

Pia wanaamini kwamba hakujiua katika kituo cha polisi alipokuwa anazuiliwa na kwamba huenda aliuawa.

Muziki wa kizito ndio chanzo cha matatizo yaliomkumba . Katika wimbo mmoja alipendekeza kwamba kila mtu aliyeuawa katika mauaji ya kimbari ya 1994 anapaswa kukumbwa awe Mtutsi ama Muhutu.

Wanasema kwamba mamlaka imeliona hilo kama changamoto ya wazi dhidi yake na kwamba mauaji hayo yalitekelezwa na Watutsi.

Wakosoaji wa serikali wanaamnini kwamba kutokana na hilo Kizito alilengwa.

Mwanamuziki huyo alikua ameanza kuchunguzwa kuhusiana na madai hayo pamoja na kutaka kuwahonga wananchi waliomkataa.

Mwaka uliopita aliachiwa huru kwa msamaha wa rais baada ya kuhukumiwa kifungo cha miaka 10 jela kwa hatia ya kutaka kumuua rais na kuhamasisha raia kupinga serikali.

Source link

,Dakika 1 iliyopita Chanzo cha picha, Reuters Maelezo ya picha, Kizito Mihigo alihoji maelezo rasmi kuhusu mauaji ya kimbari ya…

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *