Kisa Cha Mwalimu wa Chekechea Aliyesimamishwa Kufundisha Watoto KISA Michoro ya Tattoo Aliyojichora Mwili Mzima

October 6, 2020

Huko Nchini Ufaransa Mwalimu Mmoja Anayetambulika Kwa Jina Sylvain Helaine Mwenye Umri wa Miaka (35) Amesimamishwa Kuwafundisha Watoto wa chekechea Nchini humo, Baada ya Wazazi kulalamikia kuwa Michoro Iliyopo Kwenye Mwili wa Mwalimu huyo (Tattoo) Zinawatishia Watoto Hadi Kuota Ndoto Mbaya Wakiwa Usingizini.

Mwalimu huyo Ambaye Amejaza Michoro mwili Mzima hadi kwenye Ulimi huku pia Amefanya Upasuaji na kubadilisha Macho yake kuwa na Rangi Nyeusi tupu, Kwa Sasa Ameruhusiwa Kufundisha Kuanzia Wanafunzi wenye Miaka sita kwenda Juu. Sylvain Helaine Anasema Kuwa Alianza kuchora Michoro hiyo Akiwa na Umri wa miaka 27 wakati Anafundisha Nchini Uingereza Katika Mji wa London

“Napenda Tattoo, Nachora kuwaonyesha Watoto Kuwa wakiwa Wakubwa Watakutana na Watu wa Kila aina na Wanapaswa kujumuika nao, Nashangaa Wazazi wananikataza wakati Watoto wananipenda”- Sylvain Helaine

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *