Kipchoge akwama London Marathon, Ethiopia wang’aa,

October 4, 2020

 

Mbio za London zimefanyika leo Oktoba 4, 2020, ambapo Mwanariadha Shura Kitata raia wa Ethiopia ameshinda mbio hizo.

Kitata ameondoka na medali ya dhahabu baada ya kutumia muda wa Saa 02:05:41. 

Nafasi ya pili imeshikwa na Vincent Kipchumba wa Kenya ambaye ametumia muda wa 02:05:42.

Ilikuwa siku nzuri kwa taifa za Ethiopia baada ya mwanariadha mwingine kutoka nchi hiyo Sisay Lemma, kumaliza wa tatu akitumia 02:05:45.

Eliud Kipchoge amemaliza wa 8 ambapo ameeleza kuwa baada ya kilometa 25 alipata maumivu ya sikio lake la kulia na zikiwa zimebaki kilometa 15 kumaliza akapata maumivu ya nyonga hivyo kupunguza kasi yake.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *