Kiongozi wa upinzani Belarus achana pasipoti kuzuwia kufukuzwa nchini, on September 9, 2020 at 10:00 am

September 9, 2020

Maafisa nchini Belarus walijaribu kumuondoa nchini humo kwa nguvu kiongozi wa upinzaniMaria Kolesnikova lakini alichana hati yake ya kusafiria akipinga hatua hiyo na kuruka kutoka katika gari ili kubakia nchini humo, washirika wake walisema jana. Kolesnikova, mmoja wa viongozi wa mwisho ambao bado wako nchini humo wakiongoza maandamano dhidi ya rais Alexander Lukashenko, alikamatwa mpakani mapema jana baada ya kutoonekana siku ya Jumatatu. Maafisa wa mpakani wamesema alikuwa anajaribu kutoroka nchini humo lakini wenzake wawili aliokuwa nao ambao waliingia nchini Ukraine wamesema aligoma kufukuzwa nchini humo. Katika mkutano na waandishi habari katika mji mkuu wa Ukraine Kiev, katibu wa habari wa baraza la uratibu la upinzani, Anton Rodnenkov , pamoja na katibu wake mkuu Ivan Kravtsov walielezea kuhusu matukio kadhaa wakati watu hao watatu wakipelekwa mpakani.,

Maafisa nchini Belarus walijaribu kumuondoa nchini humo kwa nguvu kiongozi wa upinzaniMaria Kolesnikova lakini alichana hati yake ya kusafiria akipinga hatua hiyo na kuruka kutoka katika gari ili kubakia nchini humo, washirika wake walisema jana. 

Kolesnikova, mmoja wa viongozi wa mwisho ambao bado wako nchini humo wakiongoza maandamano dhidi ya rais Alexander Lukashenko, alikamatwa mpakani mapema jana baada ya kutoonekana siku ya Jumatatu. 

Maafisa wa mpakani wamesema alikuwa anajaribu kutoroka nchini humo lakini wenzake wawili aliokuwa nao ambao waliingia nchini Ukraine wamesema aligoma kufukuzwa nchini humo. 

Katika mkutano na waandishi habari katika mji mkuu wa Ukraine Kiev, katibu wa habari wa baraza la uratibu la upinzani, Anton Rodnenkov , pamoja na katibu wake mkuu Ivan Kravtsov walielezea kuhusu matukio kadhaa wakati watu hao watatu wakipelekwa mpakani.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *