Kiongozi wa upinzani alinganisha maandamano ya Belarus na mapambano ya Poland, on September 9, 2020 at 6:00 pm

September 9, 2020

Kiongozi mkuu wa upinzani Belarus, Svetlana Tikhanovskaya, leo ameelezea matumaini kuwa mkondo wa demokrasia nchini mwake utakuwa mfupi zaidi kuliko ulivyokuwa kwa Poland wakati wa Muungano wa Kisovieti.Akizungumza wakati wa ziara yake nchini Poland, Tikhanovyskaya amelinganisha maandamano nchini mwake na miaka mingi ya mapambano ya chama cha wafanyakazi cha Solidairity nchini Poland, ambacho kilisaidia kuuangusha ukomunisti mwaka wa 1989.Tikhanovyskaya pia amekutana na Waziri Mkuu wa Poland Mateusz Morawiecki, ambaye naye pia aliandamana dhidi ya Ukomunisti, na akazungumza na Wabelarus wanaoishi Poland.Wakati huo huo, maafisa nchini Belarus wamemkamata wakili Maxim Znak, ambaye ni mjumbe wa mwisho wa ngazi za juu wa baraza la upinzani waliokuwa wamebaki huru, ikiwa ni hatua ya kimfumo ya kuyamaliza maandamano yaliyodumu mwezi mmoja dhidi ya Rais Alexander Lukashenko.,

Kiongozi mkuu wa upinzani Belarus, Svetlana Tikhanovskaya, leo ameelezea matumaini kuwa mkondo wa demokrasia nchini mwake utakuwa mfupi zaidi kuliko ulivyokuwa kwa Poland wakati wa Muungano wa Kisovieti.

Akizungumza wakati wa ziara yake nchini Poland, Tikhanovyskaya amelinganisha maandamano nchini mwake na miaka mingi ya mapambano ya chama cha wafanyakazi cha Solidairity nchini Poland, ambacho kilisaidia kuuangusha ukomunisti mwaka wa 1989.

Tikhanovyskaya pia amekutana na Waziri Mkuu wa Poland Mateusz Morawiecki, ambaye naye pia aliandamana dhidi ya Ukomunisti, na akazungumza na Wabelarus wanaoishi Poland.

Wakati huo huo, maafisa nchini Belarus wamemkamata wakili Maxim Znak, ambaye ni mjumbe wa mwisho wa ngazi za juu wa baraza la upinzani waliokuwa wamebaki huru, ikiwa ni hatua ya kimfumo ya kuyamaliza maandamano yaliyodumu mwezi mmoja dhidi ya Rais Alexander Lukashenko.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *