Kiongozi mwingine maarufu wa upinzani akamatwa Belarus, on September 9, 2020 at 1:00 pm

September 9, 2020

 Maafisa nchini Belarus wamemkamata mjumbe wa mwisho wa ngazi za juu wa baraza la upinzani waliokuwa wamebaki huru, ikiwa ni hatua ya kimfumo ya kuyamaliza maandamano yaliyodumu mwezi mmoja dhidi ya Rais Alexander Lukashenko. Wakili Maxim Znak, mwanachama wa Baraza la Uratibu lililoundwa na upinzani kusimamia mazungumzo na kiongozi wa nchi hiyo aliyekaa madarakani kwa miaka 26 sasa, alichukuliwa katika ofisi ya baraza hilo na watu wasiojulikana waliokuwa wamefunika nyuso zao. Waendesha mashitaka wa Belarus wameanzisha uchunguzi wa jinai dhidi ya wanachama wa Baraza la Uratibu, wakilituhumu kwa kuhujumu usalama wa taifa kwa kudai uhamisho wa madaraka. Wanachama wengine kadhaa walikamatwa na wengine wakafukuzwa nchini.,

 

Maafisa nchini Belarus wamemkamata mjumbe wa mwisho wa ngazi za juu wa baraza la upinzani waliokuwa wamebaki huru, ikiwa ni hatua ya kimfumo ya kuyamaliza maandamano yaliyodumu mwezi mmoja dhidi ya Rais Alexander Lukashenko. 

Wakili Maxim Znak, mwanachama wa Baraza la Uratibu lililoundwa na upinzani kusimamia mazungumzo na kiongozi wa nchi hiyo aliyekaa madarakani kwa miaka 26 sasa, alichukuliwa katika ofisi ya baraza hilo na watu wasiojulikana waliokuwa wamefunika nyuso zao. 

Waendesha mashitaka wa Belarus wameanzisha uchunguzi wa jinai dhidi ya wanachama wa Baraza la Uratibu, wakilituhumu kwa kuhujumu usalama wa taifa kwa kudai uhamisho wa madaraka. Wanachama wengine kadhaa walikamatwa na wengine wakafukuzwa nchini.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *