Kimewaka Huko…Trump Aapa Kulipiza Mara ‘1,000’ Shambulio la Iran Dhidi ya Balozi wa Marekani

September 15, 2020

Rais wa Marekani Donald Trump ameapa kujibu mara “1,000’,” kwa shambulio lolote la Iran.Hii ni baada ya taarifa kwamba Iran ilikuwa inapanga kumuua balozi wa Marekani nchini Afrika Kusini, Lana Marks.”Shambulio lolotela Iran, la muundo wowote, dhidi ya Marekani litakutana na shambulio dhidi ya Iran ambalo litakuwa ni kubwa mara 1,000 !” Bwana Trump alitweet Jumatatu.Msemaji wa Wizara ya mambo ya nje wa Iran Saeed Khatibzadeh amepuuzilia mbali taarifa juu ya mpango wa mauaji ambao kwanza uliripotiwa na Politico.Iliripoti kuwa Iran ilikuwa inapanga kumuua Balozi wa Marekani, ambaye ni rafiki wa muda mrefu wa Rais Trump, katika hatua yake ya kujibu mauaji ya Jenerali Qasem Soleimani mwezi januari.Gen Soleimani aliuawa katika shambulio za ndege za Marekani zisizokuwa na rubani Baghdad mwezi Januari.,

Rais wa Marekani Donald Trump ameapa kujibu mara “1,000’,” kwa shambulio lolote la Iran.
Hii ni baada ya taarifa kwamba Iran ilikuwa inapanga kumuua balozi wa Marekani nchini Afrika Kusini, Lana Marks.

“Shambulio lolotela Iran, la muundo wowote, dhidi ya Marekani litakutana na shambulio dhidi ya Iran ambalo litakuwa ni kubwa mara 1,000 !” Bwana Trump alitweet Jumatatu.

Msemaji wa Wizara ya mambo ya nje wa Iran Saeed Khatibzadeh amepuuzilia mbali taarifa juu ya mpango wa mauaji ambao kwanza uliripotiwa na Politico.

Iliripoti kuwa Iran ilikuwa inapanga kumuua Balozi wa Marekani, ambaye ni rafiki wa muda mrefu wa Rais Trump, katika hatua yake ya kujibu mauaji ya Jenerali Qasem Soleimani mwezi januari.

Gen Soleimani aliuawa katika shambulio za ndege za Marekani zisizokuwa na rubani Baghdad mwezi Januari.,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *