Kimbunga Sally chapiga majimbo ya Alabama na Florida, on September 17, 2020 at 10:00 am

September 17, 2020

Kimbunga Sally kimepiga mwambao wa karibu na mpaka baina ya majimbo ya Alabama na Florida Kusini mwa Marekani, kikiambatana na mafuriko na upepo unaokwenda kwa kasi ya km 165 kwa saa. Mamia ya watu wamelazimika kuokolewa baada ya nyumba zao kujaa maji. Kimbunga hicho kimesomba maboti yaliyokuwa ufukweni na kuyatupa nchi kavu, na kuangusha miti na kuezua nyumba katika miji ya Pensacola na Mobile. Nyumba zipatazo 540,000 za makaazi ya watu na biashara zimeachwa bila umeme katika eneo hilo la kaunti ya Escambia, ambako maafisa wamesema watu 377 wameokolewa kutoka nyumba zilizofurika maji, ikiwemo familia ya watu wanne ambao walikuwa wamepanda mitini kuepuka kumezwa na mafuriko. Hali ya hatari imetangazwa katika baadhi ya miji ya mwambao katika jimbo la Alabama, wakati vikosi vya kitaifa vya uokozi vikisubiriwa kuwasili katika majimbo yaliyoathiriwa.,

Kimbunga Sally kimepiga mwambao wa karibu na mpaka baina ya majimbo ya Alabama na Florida Kusini mwa Marekani, kikiambatana na mafuriko na upepo unaokwenda kwa kasi ya km 165 kwa saa. 

Mamia ya watu wamelazimika kuokolewa baada ya nyumba zao kujaa maji. Kimbunga hicho kimesomba maboti yaliyokuwa ufukweni na kuyatupa nchi kavu, na kuangusha miti na kuezua nyumba katika miji ya Pensacola na Mobile. 

Nyumba zipatazo 540,000 za makaazi ya watu na biashara zimeachwa bila umeme katika eneo hilo la kaunti ya Escambia, ambako maafisa wamesema watu 377 wameokolewa kutoka nyumba zilizofurika maji, ikiwemo familia ya watu wanne ambao walikuwa wamepanda mitini kuepuka kumezwa na mafuriko.

 Hali ya hatari imetangazwa katika baadhi ya miji ya mwambao katika jimbo la Alabama, wakati vikosi vya kitaifa vya uokozi vikisubiriwa kuwasili katika majimbo yaliyoathiriwa.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *