Kikwete: Wanaosema mikoa ya kanda ya Kusini imesahauliwa na imeachwa nyuma hawaijui mikoa hiyo, on September 8, 2020 at 6:04 pm

September 8, 2020

. Na Ahmad Mmow, LindiRais mstahafu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania wa awamu ya nne, Dkt Jakaya Kikwete amesema wanasiasa na wagombea wanaosema mikoa ya Lindi na Mtwara imesahauliwa na imeachwa nyuma kimaendeleo hawaijui mikoa hiyo na waongo.Dkt Kikwete ameyasema hayo katika uzinduzi wa kampeni za uchaguzi katika mkoa wa Lindi kwa wagombea wanaopitia Chama Cha Mapinduzi(CCM). Uzinduzi ambao umefanyika leo katika uwanja wa mpira wa miguu wa Ilulu, manispaa ya Lindi.Alisema hakuna Mkoa wowote ambao unavitu vyote. Kwani mambo ambayo yamefanyika katika mikoa hiyo yanaweza kuwa yasiwepo mikoa mingine. Hali kadhalika yaliyopo katika mikoa mingine hayapo katika mikoa hiyo ya Lindi na Mtwara. Kwahiyo siyo kweli kwamba mikoa hiyo imeachwa nyuma na imesahauliwa. Kwahiyo wanaosema hiyo uhenda hawaijui au wameamua kupotosha kwa makusudi.Kikwete ambaye alitaja mambo mengi yaliyofanyika katika mikoa hiyo ikiwamo miradi ya maendeleo alisema mambo yaliyofanyika yanaoneka dhahiri na mabadiliko ni makubwa. Kwani yanayoonekana katika mikoa hiyo hayakuwepo.Rais mstahafu huyo wa awamu ya nne alitolea mfano wilaya ya Nachingwea jinsi ilivyobadilika kimaendeleo. Akibainisha kwamba alipokuwa katibu wa CCM wa wialaya hiyo mwaka 1986 ilikuwa siyo jambo la ajabu kusikia watu wameliwa na Simba au kutembea bila kukutanana nyoka. Lakini hivi sasa Nachingwea imebadilika na inamaendeleo makubwa. Hayo ya Simba na nyoka yamebaki kuwa ni historia.Kuhusu miundombinu katika mikoa hiyo alisema hali ya barabara ilikuwa mbaya. Hasa kutoka katika mikoa hiyo kwenda Dar-es-Salaam. Hata hivyo tatizo hilo limekwisha. Kwani hivi sasa kuna barabara ya lami. Barabara ambayo ujenzi wake ulianza katika awamu ya tatu ya utawala chini ya hayati Benjamin Mkapa. Ambapo katika utawala wake yeye alimalizia.Alisema kazi ya kuleta maendeleo kwa wananchi ni endelevu. Hata hivyo mambo mengi yamefanyika na yanaonekana, lakini baadhi ya wagombea na wanasiasa hawataki kuyasema kutokana na hofu ya kuharibikiwa dhamira zao.” Kwamiaka mitatu mfululizo mkoa wa Lindi ilikuwa kinara kwa matokeo ya kidato cha nne na sita. Lakini hawataki kusema, wanakumbusha mambo ya zamani ambayo hayana mahusiano na hali ilivyo. Hata matatizo ya korosho yamerekebishwa hayapo lakini kwakuwa wamekosa hoja wanasema hata yazamani,” alisema Kikwete.Aidha Kikwete alisema kunakila sababu ya wananchi kuchagua CCM kiendelee kuwa chama tawala kutokanana kusimamia na kuendeleza amani, utulivu na mshikamano. Mambo ambayo yanasababishwa na sera unganishi na jumuishi. Huku akiweka wazi kwamba bila sera jumuishi na unganishi  kungekuwa na migogoro.Alisema licha ya Tanzania kuwa na watu wengi, eneo kubwa na watu wenye itikadi za vyama tofauti, dini tofauti na makabila tofauti takribani 120 lakini wananchi wanaendelea kuwa wamoja na wanaishi kama ndugu. Kwahiyo kunahaja ya kukipa ridhaa CCM kiendelee kutawala na kuunda serikali.,

. Na Ahmad Mmow, Lindi

Rais mstahafu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania wa awamu ya nne, Dkt Jakaya Kikwete amesema wanasiasa na wagombea wanaosema mikoa ya Lindi na Mtwara imesahauliwa na imeachwa nyuma kimaendeleo hawaijui mikoa hiyo na waongo.

Dkt Kikwete ameyasema hayo katika uzinduzi wa kampeni za uchaguzi katika mkoa wa Lindi kwa wagombea wanaopitia Chama Cha Mapinduzi(CCM). Uzinduzi ambao umefanyika leo katika uwanja wa mpira wa miguu wa Ilulu, manispaa ya Lindi.

Alisema hakuna Mkoa wowote ambao unavitu vyote. Kwani mambo ambayo yamefanyika katika mikoa hiyo yanaweza kuwa yasiwepo mikoa mingine. Hali kadhalika yaliyopo katika mikoa mingine hayapo katika mikoa hiyo ya Lindi na Mtwara. Kwahiyo siyo kweli kwamba mikoa hiyo imeachwa nyuma na imesahauliwa. Kwahiyo wanaosema hiyo uhenda hawaijui au wameamua kupotosha kwa makusudi.

Kikwete ambaye alitaja mambo mengi yaliyofanyika katika mikoa hiyo ikiwamo miradi ya maendeleo alisema mambo yaliyofanyika yanaoneka dhahiri na mabadiliko ni makubwa. Kwani yanayoonekana katika mikoa hiyo hayakuwepo.

Rais mstahafu huyo wa awamu ya nne alitolea mfano wilaya ya Nachingwea jinsi ilivyobadilika kimaendeleo. Akibainisha kwamba alipokuwa katibu wa CCM wa wialaya hiyo mwaka 1986 ilikuwa siyo jambo la ajabu kusikia watu wameliwa na Simba au kutembea bila kukutanana nyoka. Lakini hivi sasa Nachingwea imebadilika na inamaendeleo makubwa. Hayo ya Simba na nyoka yamebaki kuwa ni historia.

Kuhusu miundombinu katika mikoa hiyo alisema hali ya barabara ilikuwa mbaya. Hasa kutoka katika mikoa hiyo kwenda Dar-es-Salaam. Hata hivyo tatizo hilo limekwisha. Kwani hivi sasa kuna barabara ya lami. Barabara ambayo ujenzi wake ulianza katika awamu ya tatu ya utawala chini ya hayati Benjamin Mkapa. Ambapo katika utawala wake yeye alimalizia.

Alisema kazi ya kuleta maendeleo kwa wananchi ni endelevu. Hata hivyo mambo mengi yamefanyika na yanaonekana, lakini baadhi ya wagombea na wanasiasa hawataki kuyasema kutokana na hofu ya kuharibikiwa dhamira zao.

” Kwamiaka mitatu mfululizo mkoa wa Lindi ilikuwa kinara kwa matokeo ya kidato cha nne na sita. Lakini hawataki kusema, wanakumbusha mambo ya zamani ambayo hayana mahusiano na hali ilivyo. Hata matatizo ya korosho yamerekebishwa hayapo lakini kwakuwa wamekosa hoja wanasema hata yazamani,” alisema Kikwete.

Aidha Kikwete alisema kunakila sababu ya wananchi kuchagua CCM kiendelee kuwa chama tawala kutokanana kusimamia na kuendeleza amani, utulivu na mshikamano. Mambo ambayo yanasababishwa na sera unganishi na jumuishi. Huku akiweka wazi kwamba bila sera jumuishi na unganishi  kungekuwa na migogoro.

Alisema licha ya Tanzania kuwa na watu wengi, eneo kubwa na watu wenye itikadi za vyama tofauti, dini tofauti na makabila tofauti takribani 120 lakini wananchi wanaendelea kuwa wamoja na wanaishi kama ndugu. Kwahiyo kunahaja ya kukipa ridhaa CCM kiendelee kutawala na kuunda serikali.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *