Kikosi kipya cha polisi chaundwa kuchukua nafasi ya kikosi ‘katili’ Nigeria,

October 14, 2020

 

Kiosi maalumu cha kupambana na wiziSpecial Anti-Robbery Squad -kilishutumiwa kwa ukatiliImage caption: Kiosi maalumu cha kupambana na wiziSpecial Anti-Robbery Squad -kilishutumiwa kwa ukatili

Mkuu wa polisi nchini Nigeria amesema kikosi kipya kimeundwa ili kuchukua nafasi ya kikosi tata maalumu cha polisi cha kukabiliana na wizi kinachofahamika Sars, ambacho kilivunjwa kufuatia maandamano ya ukiukaji wa haki za binadamu dhidi yake.

Waandishi wa habari wanasema Wanigeria wengi hawana Imani na wanaendelea kuandamana wakitaka yafanyike mageuzi makubwa katika polisi ya nchi hiyo.

Katika juhudi za kutatua kuondoa hofu miongoni mwa Wanigeria mkuu wa polisi amesema kuwa polisi wote kutoka katika kikosi kilichovunjwa watapitia uchunguzi wa kisaikolojia na kimatibabu kabla ya kupata mafunzo zaidi na kupelekwa tena katika sehemu za kazi.

Pia aliagiza kuachiliwa huru bila masharti yoyote kwa watu wote waliokamatwa wakati wa maandamano.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *